Jengo la OPCW lililoko mjini The
Hague Uholanzi
Tuzo ya amani ya Nobel mwaka wa 2013
imeliendea shirika la kimataifa la kudhibiti silaha za kemikali OPCW, kutokana
na juhudi zake kubwa za kuangamiza silaha za sumu.
Kulingana na mwenyekiti wa Kamati ya Norway ya Nobel Thorbjoern Jagland, wametoa tuzo
kwa shirika hilo
kutokana na namna inavyoshughulikia uangamizi wa silaha hatari za nyuklia.
Shirika hilo lililoundwa mwaka wa 1997 lilitwikwa
jukumu la kuondoa na kuangamiza kabisa silaha za sumu duniani kote. Tuzo hiyo
ambayo inajumuisha zawadi nono ya kitita cha dola milioni 1.25 ilitangazwa muda
mfupi uliopita mjini Oslo Norway.
Baadaye Disemba 10 shirika hilo linatarajiwa kukabidhiwa rasmi tuzo hiyo huko huko
mjini Oslo
ambako pia itakuwa ni siku aliyofariki muanzilishi wa tuzo hiyo, Alfred Nobel.
Tuzo ya amani ya Nobel imekuwa ikitolewa tangu mwaka wa 1985.
Viongozi wa shirika la OPCW Viongozi
wa shirika la OPCW
Kulingana na msemaji wa OPCW Michael
Luhan, tangu shirika hilo
lilipoundwa miaka 16 iliopita limeharibu takriban tani 57,000 za kemikali ya
nyuklia, nyingi zikiwa zile zilizoachwa katika vita baridi vya Marekani na
Urusi.
Shirika hilo lenya wanachama nchi 189 na lililo na
makao yake makuu mjini The Hague, Uholanzi, lina takriban wafanyakazi 500.
Umuhimu wa shirika hilo
ulionekana zaidi mwaka huu baada ya gesi yenye sumu ya Sarin kutumika mjini Damascus mwezi Agosti na
kusababisha mauaji ya takriban watu 1,400.
Marekani moja kwa moja ilimshutumu
rais wa Syria, Bashar Al
Assad, kwa kutumia silaha hizo, shutuma ambazo alikazinusha vikali na kusema
waasi ndio waliotumia gesi ya sumu dhidi ya raia wa Syria.
OPCW yasema Syria yatoa
ushirikiano mkubwa
Baada ya Assad kukumbwa na vitisho
kutoka Marekani kwamba huenda nchi hiyo ikaingilia kijeshi kutokana na matumizi
ya silaha hizo, Assad alikubali kuharibu silaha zake zote za Nyuklia na kutoa
fursa kwa wataalamu wa shirika la OPCW kuingia nchini humo na kutekeleza
majukumu yao.
Wataalamu wa OPCW nchini Syria
Wataalamu wa OPCW nchini Syria
Hata hivyo shirika la OPCW, linasema Syria imeamua
kutoa ushirikiano na huenda silaha za kemikali za nchi hiyo zikaangamizwa
katikati ya mwaka 2014.
Hata hivyo, Hamish De Bretton,
mtaalamu wa maswala ya Nyuklia anasema shirika hilo limestahili kupokea tuzo hiyo lakini
linakabiliwa na changamoto kubwa.
"Hii ni tuzo nzuri kabisa kwa
shirika la OPCW lakini kutokana nan kile kitakachoonekana nchini Syria kwa
mwezi ujao ama siku chache zijazo nmi muhimu sana na bila kupata uungwaji mkono
wa upinzani nadhani itakuwa jukumu lililo na changamoto kubwa," Alisema
Hamish de Bretton.
Kwa miaka miwili mfululizo tizo ya
amani ya Nobel imetuzwa kwa mashirika, mwaka uliopita shirika la Umoja wa Ulaya
lilivikwa taji hiyo ya tuzo ya amani ya Nobel.
Mwandishi: Amina Abubakar/Reuters/AP
Mhariri: Josephat Charo
Chanzo: DW.DE
No comments:
Post a Comment