Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania
(TCAA), imesema ajira ya marubani wazalendo ipo mashakani kwa sababu ndege
nyingi nchini, zinaongozwa na wageni.TCAA imesema hali hiyo imekuwa ikichangiwa
na kampuni zinazotoa huduma hizo nchini, kutumia ndege nyingi za kukodi
zinazofanya kazi chini ya masharti yanayotoa nafasi kubwa ya kuongozwa na
marubani wa kigeni.
"Ndege ni ghali sana na wengi walioko kwenye sekta hii
wanakopeshwa na kupewa masharti,"alisema Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Fadhili
Manongi, alipokuwa akizungumza katika mahojiano na gazeti hili.
Alisema karibu asilimia 50 ya
marubani wanaoendesha ndege zinazofanya kazi hapa nchini, ni wa kigeni.
Manongi alisema ingawa mikataba
kuwabana, kigezo cha uzoefu pia ni kikwazo kwa marubani wengi wazalendo.
"Wengine wanashindwa kupata
ajira kutokana na kutokuwa na saa zinazohitajika ili mtu aweze kurusha ndege za
biashara," alisema.
Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, kwa
sasa Tanzania
ina marubani 500 na katika miaka mitatu ijayo watafikia 700.
Alisema kwa jumla sekta ya usafiri wa
anga ina upungufu wa wataalamu kama wahandisi
na marubani lakini shida kubwa inawahusu zaidi marubani.
Manongi alisema kwa kuzingatia hali
hiyo, TCAA ipo kwenye mikakati ya kuboresha sekta ya marubaini nchini ili
pamoja na mafunzo, pia wapate uzoefu utakaowawezesha kutoa ushindani kwenye
soko la ajira ndani na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment