Dodoma. Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wameaswa wasinakili tu michakato ya Kikatiba toka nchi nyingine, kwani yale yafanywayo huko hayataakisi wala kukidhi matakwa ya Watanzania.
Hayo yalibainishwa na Mwanasheria
Mkuu wa zamani wa Kenya, Amos Wako mjini Dodoma leo, wakati akielezea yale
Kenya iliyokumbana nayo wakati ikiandika Katiba yake mpya.
“Mnaposikiliza uzoefu wa nchi
nyingine, tafadhali msiwanakili, msije mkarudia makosa yao,” alisema Wako
ambaye hivi sasa ni Seneta wa Kaunti ya Busia, akiongeza: “Hata kama mmependa
waliyoyafanya, yawezekana yasiwafae [Watanzania].”
Vilevile, Bw. Wako aliipongeza
Tanzania kwa kuwa tayari kupeleka mapendekezo ya Bunge Maalum la Katiba moja
kwa moja kwa wananchi, akisisitiza kuwa uamuzi huo utazuia rasimu isije
ikachakachuliwa na wanasiasa.
“Kama [rasimu] ingepitiwa na chombo
kingine [kabla ya kwenda kwa wananchi], yawezekana ikafanyiwa mabadiliko yasiyo
na maslahi [kwa umma],” alisema nguli huyo wa sheria.
Ungepende kufahamu kilichojiri baada
ya hotuba ya Wako? Je, Mchungaji Christopher Mtikila aliibua suala gani leo?
Tazama VIDEO ufahamu mengine
yalotokea leo Dodoma.
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment