Paris inapata meya wake wa kwanza
mwanamke lakini chama chake tawala cha Socialistics kilipata kipigo katika
mzunguko wa pili wa uchaguzi wa serikali za mitaa nchini Ufaransa.
Anne Hidalgo mzaliwa wa Spain
alimshinda mpinzani wake m-conservative kushinda wadhifa wa cheo cha juu katika
mji mkuu wa Ufaransa.
Hidalgo awali alihudumu kama naibu wa
meya anayemaliza muda wake, Betrand Delanoe. Alishinda kwa ahadi ya kujenga
nyumba mpya za umma na kurahisisha zaidi mfumo wa huduma ya kulea watoto kwa
familia za Paris.
Waangalizi wengi wa kisiasa
wanaiangalia ofisi ya meya wa Paris kama hatua moja kusonga mbele kwa urais wa
Ufaransa.
Lakini chama cha Hilalgo cha
Socialists hakikufanya vyema katika miji na miji mikubwa mingi mingine ya
Ufaransa, imepoteza uungaji mkono kwa
wanaopinga uhamiaji na wanaopinga chama cha European Union national Front.
Uchaguzi unaonekana kama kura ya
maoni kwa rais asiye maarufu, Francois Hollande.
Wapiga kura wamekasirishwa na
kudorora kwa uchumi na kiwango cha juu cha ukosefu wa ajira. Chanzo: VOA
Wasoshialisti
waondolewa patupu Ufaransa
Mji mkuu wa Ufaransa Paris umejipatia meya wa kwanza
mwanamke:Anne Hidalgo wa chama cha kisoshialisti
Siku moja tu baada ya wasoshilisti
kushindwa vibaya sana katika uchaguzi wa mabaraza ya miji ya Ufaransa,rais
Francois Hollande anashinikizwa na kila upande aivunje serikali na abadilishe
pia mkondo wa siasa yake.
"Rais amevuliwa nguo" ndio
kichwa cha maneno cha gazeti la mrengo wa shoto La Liberation linalohisi rais
Hollande ambae hapendi kupitisha uamuzi kwa pupa,hawezi tena kukwepa na
"anabidi afichue haraka kile anachodhamiria kufanya."
"Zilzala,pigo,adhabu,hatakiwi"
ni miongoni mwa vichwa vya maneno katika magazeti ya Ufaransa yanayotoa picha
ya janga linalomgubika rais Hollande baada ya uchaguzi huu ambao ni wa kwanza
tangu aingie madarakani mwezi Mai mwaka 2012.
Kambi ya wasoshialisti imepokonywa na
wahafidhina miji isiyopungua 155 yenye wakaazi zaidi ya 9000-na baadhi ya miji
hiyo ilikuwa ikiongozwa na mrengo wa shoto kwa zaidi ya miaka 100.
Sauti zinazidi kupazwa waziri mkuu
abadilishwe
Kutoka kushoto:rais Hollande,waziri
mkuu Ayrault na waziri wa masuala ya haki za akinamama ambae pia ni msemaji wa
serikali Nadjat Vallaud Belkacem
Kutoka kushoto:rais Hollande,waziri
mkuu Ayrault na waziri wa masuala ya haki za akinamama ambae pia ni msemaji wa
serikali Nadjat Vallaud Belkacem
Miito kutaka waziri mkuu abadilishwe
imezidi kupata nguvu sio tu kutoka kambi ya wahafidhina bali pia mrengo wa
shoto. Jean-Marc Ayrault anatwikwa jukumu la kushindwa siasa ya serikali ya
Ufaransa tangu takriban miaka miwili iliyopita.
Kwa mujibu wa utafiti wa maoni
ya wananchi uliosimamiwa na taasisi ya BVA,zaidi ya robo tatu ya wafaransa
wasingependelea kumuona Jean Marc Ayrault akiendelea kuongoza serikali.
Wakaribu wa rais Francois Hollande
wamesema wazi jana usiku "ujumbe wameupata".Rais Francois Hollande
anatazamiwa kulihutubia taifa leo hii."Wapiga kura wameelezea hisia
zao...na baadhi ya wakati kwa hasira" amesema hayo waziri wa mambo ya
ndani Manuel Valls anaepewa nafasi nzuri ya kuteuliwa kuwa waziri mkuu
mpya.Amekiri matokeo ya uchaguzi wa jana ni pigo kwa chama cha kishoshiliasti
tangu katika daraja ya kimkoa mpaka kitaifa.
Manuel Valls alikuwa akutane na rais
Francois Hollande leo asubuhi kabla ya rais Hollande kuzungumza na waziri mkuu
Jean-Marc Ayrault.
Jean Marc Ayrault ameungama anabeba
shemu ya dhamana ya pigo hilo linaloashiria na mengine yanaweza kufuata mfano
katika uchaguzi wa bunge la ulaya mwezi May ujao na ule wa baraza la senet
ambao unaweza kupibndua wizanio wa nguvu na kuelemea mrengo wa kulia.
Mnara wa Eifel:Kivutio cha watalii
mjini Paris
Pigo la uchaguzi limechanganyika na
ripoti zilizochapishwa leo kuhusu kuongezeka nakisi ya bajeti ya nchi
hiyo.Katika wakati ambapo lengo lilikuwa kuipunguza hadi asili mia 4.1 ya pato
la ndani kwa mwaka 2013 dhidi ya asili mia 4.9 mwaka 2012,nakisi hiyo imefikia
asili mia 4.3.
Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Reuters/AFP
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman
No comments:
Post a Comment