Ujumbe wa askari wa Jeshi la Polisi la Uganda
umewasili nchini kwa kile kinachodaiwa kuja kufanya mazungumzo ili kupata
maridhiano kufuatia kitendo cha askari wake wakiwa na bunduki kuvamia eneo la
Mutukula, mkoani Kagera, na kurusha risasi ovyo zilizojeruhi Watanzania wawili.
Habari zilizopatikana jana zinaeleza
kuwa askari hao ujumbe wa askari hao umewasili nchini wakiongozwa na mmoja wa
viongozi wakuu wa Jeshi la Polisi Mbarara, nchini humo.
NIPASHE, ambayo ilifika katika Kituo
Kikuu cha Polisi jana asubuhi iliwashuhudia askari wanne wa Uganda waliovalia
sare, wakiwa nje ya kituo hicho, ambako mwenzao mmoja anashikiliwa kwa tuhuma
hizo.
Hata hivyo, habari nyingine zilieleza
kuwa mbali na kuja kutafuta maridhiano baina yao na wenzao wa Tanzania, ujumbe
huo pia umekuja nchini kwa ajili ya kumchukulia dhamana mwenzao anayeshikiliwa
na polisi wa Tanzania.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, George
Mayunga, alipotakiwa jana kuelezea suala hilo, alisema hadi jana alikuwa
hajapata kibali cha kuzungumzia suala hilo kutoka Makao Makuu ya Polisi, jijini
Dar es Salaam.
Msemaji wa Jeshi hilo nchini, Advera
Senso, jana hakupatikana kuzungumzia kinachoendelea kuhusiana na kadhia hiyo na
hata alipopigiwa simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita bila kupokelewa.
Hata hivyo, juzi alikaririwa akisema
kinachopfanywa na Jeshi la Polisi ni kuchunguza ili kujua sababu za askari hao
kuendesha operesheni hiyo nchini bila kuwaarifu wenzao wa Tanzania kama sera ya
Interpol (Polisi wa Kimataifa) inavyotaka.
Askari saba kutoka Uganda Jumamosi
wiki iliyopita wakiwa na silaha hizo, walivamia eneo hilo kwa kile kilichodaiwa
kuwa walikuwa wakiwatafuta watuhumiwa wa wizi wa pikipiki waliokimbilia
Tanzania.
Chanzo: Nipashe
No comments:
Post a Comment