Serikali ya Ufaransa imetangaza kuwa
inajiondoa katika maadhimisho ya miaka 20 tangia mauaji ya halaiki nchini
Rwanda.
Uamuzi huo unafuatia shtuma kutoka
kwa rais wa taifa hilo Paul kagame kwamba Ufaransa ilishiriki katika mauaji
hayo ya kimbari mnamo mwaka 1994.
Rais Kagame aliwahi kutoa madai kama
hayo hapo awali.
Msemaji wa wizara ya maswala ya
kigeni nchini Ufaransa Romain Nadal amesema kuwa matamshi hayo yanaenda kinyume
na harakati za maridhiano kati ya mataifa hayo mawili.
Amesema kuwa waziri wa maswala ya
haki Christiane Taubira alivunjilia mbali ziara yake ya kushiriki katika
maadhimisho hayo mjini Kigali siku ya jumatatu.
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment