Waziri mkuu nchini Mali Oumar Tatamy
Ly pamoja na baraza lake la mawaziri wamejiuzulu,miezi minane tu baada ya
demokrasia kurudi nchini humo kufuatia udhibiti wa eneo la kazkazini
uliotekelezwa na wanamgambo wa kiislamu.
Mabadiliko katika serikali yalitarajiwa
kufanyika ,lakini mwandishi wa BBC katika mji mkuu wa Mali Bamako,anasema kuwa
kiwango cha mabadiliko hayo hakikutarajiwa.
Waziri mkuu mpya ,Moussa Mara amekuwa
mpinzani mkuu wa rais Boubakr Keita hapo awali.
Bwana Mara aliye na umri wa miaka 39
amekuwa akiitaka serikali kuimarisha usalama katika eneo la kazkazini la nchi
hiyo.
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment