Friday, April 4, 2014

Tanzania: Mvutano wazuka juu ya hati ya Muungano

                           Mwalimu Julius K.Nyerere, mwasisi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Nchini Tanzania kuna utata ulozuka kuhusu kugushiwa kwa saini za Mwalimu Julius Nyerere na Pius Msekwa.
Suala la kugushiwa kwa saini ya mmoja kati ya waasisi wa muungano hayati, Mwalimu Julius Nyerere na sehemu ya saini ya aliyekuwa Katibu wa Bunge la Tanganyika, Pius Msekwa zilizopo kwenye hati ya sheria ya kuridhia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar limekuwa kama kikwazo kingine katika maendeleo ya mijadala ya bunge la katiba. 

Sudi Mnette amezungumza na Richard Shaba kutoka wakfu wa Konrad Adenauer nchini Tanzania.Kwanza alitaka kujua hali ya kutoonekana hasa kwa hati halisi ya muungano kama invyohitajika katika bunge la katiba anaizungumziaje?
Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za maskioni hapo chini.
http://www.dw.de/tanzania-mvutano-wazuka-juu-ya-hati-ya-muungano/a-17543561 
Mwandishi: Sudi Mnette
Mhariri: Mohammed Abdulrahman

No comments: