Polisi wa Kenya wakikagua eneo lililoshambuliwa la kanisa huko Mombasa. March 23, 2014.
VOA NAIROBI
Milipuko mitatu katika mji mkuu wa
Kenya wa Nairobi imesababisha vifo vya watu 6 na karibu darzeni mbili
kujeruhiwa jumatatu usiku katika mtaa mkubwa wenye wakazi wengi wa asili ya
Kisomali wa Eastleigh.
Mkuu wa polisi wa County ya Nairobi
Benson Kibue anasema milipuko hiyo ilitokea takriban saa moja na nusu
usiku na kwa karibu wakati mmoja katika
migahawa ya Sheraton Café na The New Kwa muzairua Grill.
Kufuatana na mmiliki wa Sheraton Café
Bw. Patrick Gakuyu watu walikuwa wanatizama taarifa ya habari ya saa moja
kwenye televisheni wakati aliposikia milipuko miwili na umeme kuzimika na kuwa
katika kiza. Anasema anadhani ni grunetti mbili zilizorushwa ndani ya mgahawa
wake.
Jumapili usiku karibu na mtaa huo mtu
anayedhaniwa ni gaidi aliuwawa alipokuwa anatengeneza milipuko yake pamoja na
wenzake watatu. Na gruneti moja ilipatikana siku hiyo hiyo ya jumapili katika
mji wa pwani wa Lamu ndani ya kanisa moja.
Usalama umeimarishwa katika miji
mikuu ya Kenya na hadi hivi sasa haijulikani aliyehusika na mashambulio ya
jumatatu.
BBC NAIROBI
Watu sita wameuawa na wengine wengi
kujeruhiwa katika shambulizi la kigaidi katika eneo la California mtaa wa
Eastleigh, mjini Nairobi.
Polisi wamesema kuwa milipuko miwili
ilitokea wakati magaidi waliporusha mabomu katika mkahawa mdogo ulio karibu na
kituo cha mabasi mtaani humo.
Polisi mtaani Eastleigh
Walioshuhudia shambulizi walisema
kuwa walisikia mlipuko wa tatu katika eneo hilo ingawa polisi hawajathibitisha
hilo.
Miongoni mwa waliojeruhiwa walikuwa
wanawake ambao walipata majeraha mabaya na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu.
Kwa mujibu wa polisi wale waliouawa
walikuwa wamekwama ndani ya mkahawa huo baada ya mlango kufungwa na
washambulizi waliorusha mabomu hayo ndani ya mkahawa wenyewe.
Waathiriwa walikuwa wameenda kununua
chakula cha jioni. Idadi kubwa ya wakimbizi wa Somali wanaishi katika mtaa wa Eastleigh.
Inaarifiwa washambuliaji walitumia
maguruneti au mabomu ya kutengezwa nyumbani kufanya mashambulizi hayo.
No comments:
Post a Comment