Rais Uhuru Kenyatta
Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC
imehairisha kesi dhidi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta hadi tarehe saba Oktoba
mwaka huu.
Rais Kenyatta anashtumiwa kwa makosa
ya jinai kufuatia machafuko ya baada ya uchaguzi wa mkwaka 2007 - 2008, madai
ambayo ameyakanusha.
Mahakama kuu ya ICC, kupitia
mwendesha mashtaka Fatou Bensouda, imekuwa ikiitaka serikali ya Kenya kutoa
ushirikiano wa kutosha ili kuendesha kesi zinazowakabili Rais Kenyatta na naibu
wake
bwana Ruto.
Hii ni mojawapo za sababu kuu za
kubadili tarehe za kusikizwa kwa kesi hii.
Upande wa mashtaka umesema kuwa
unaipa Kenya muda wa ziada ili kutafuta na kuwasilisha baadhi ya stakabadhi za
benki zinazohitajika katika kesi hiyo.
Kumekuwa na malalamishi kutoka kwa
upande wa mashtaka kuwa serikali ya Kenya inalenga kuzuia stakabadhi hizo
kufikishwa mahakamani jambo ambala mawakili wa bwana Kenyatta wamekanusha.
Miongoni mwa yale yanayohitajika
kotini ni pamoja na taarifa ya maelezo ya fedha anazomiliki bwana Kenyatta.
Kesi hii imekumbwa na matatizo ya
mashahidi kujiondoa na shutuma za mahakma hii kuonea viongozi wa bara Afrika.
No comments:
Post a Comment