Leo unatimia mwaka mmoja tokea Rais
Uhuru Kenyatta aanze kuiongoza Kenya.Katika hotuba yake ya kuingia madaraka
Kenyatta alitoa ahadi nyingi. Jee amezitekeleza kwa kiasi gani. Ni mwaka mmoja,
tokea Rais Kenyatta aapishwe kuanza kulitumikia taifa la Kenya .
Alitoa ahadi nyingi; ikiwa pamoja na
kuuendeleza uchumi, kuuimarisha umoja wa taifa na kuweka utaratibu wa huduma za
afya zinazoweza kulipiwa na kila mwananchi .Rais Kenyatta pia aliahidi kuleta
uhakika wa chakula, kutenga nafasi za ajira kwa vijana na kugawa
"Laptop" kwa watoto wote wa shule za msingi.Lakini aliyoweza
kuyafanya ili kuzitekeleza ahadi hizo ni machache hadi sasa.
Bei za vyakula zimezidi kupanda,
ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana bado ni wa kiwango cha juu na hasa katika
sehemu za mashambani .Aidha mpango wa kugawa "Laptop" kwa watoto wa
shule umesahauliwa ndani ya mtoto wa meza kufuatia kashfa.
Mwandishi habari mmoja Inchikirwa
Ndelejai amesema serikali ya Kenyatta haijafanya mengi. Amesema serika ya
mfungamano wa Jubilee haijafanya ya kutosha. Ameeleza kwamba serikali
haikufanya kama ilivyoahidi.
Mwandishsi habari huyo amesema ,ikiwa
mtu atawapima wanasiasaa katika msingi wa ahadi walizozitoa, basi
kilichofanyika hadi sasa ni cha kusikitisha.
Hatua fulani zapigwa
Hata hivyo hatua kadhaa zimepigwa na
serikali ya Kenyatta katika kuzitekeleza baadhi ya ahadi. Mara tu baada ya
kuchaguliwa Kenyatta alianza kuutekeleza utaratibu wa kutoa huduma kwa ajili ya
wajawazito bila ya malipo.Akina mama hawalipii gharama za kupimwa wanapokuwa
wajawazito na pia hawalipii gharama za kujifungua.Katika hotuba yake Rais
Kenyatta ,alisifu mafanikio yaliyopatikana katika uchumi na hatua
zilizochukuliwa katika kupambana na ufisadi.
Hatua fupi katika kupambana na
ufisadi
Hata hivyo kuhusu ufisadi ndani ya
polisi,mwakilishi wa Wakfu Ujerumani wa " Heinrich Böll" nchini Kenya
Katrin Seidel amesema kwamba maafisa wengi wa polisi waliohusika na vitendo vya
ufisadi vilivyoweza kuthibitishwa bado wanaendelea na kazi na bado wamo katika
ngazi za uongozi pia katika idara ya usalama. Mwakilishi huyo wa Wakfu wa
Ujerumani ,bibi Seidel amesema watu wengi nchini Kenya wanahisi kwamba
hawahudumiwi kwa kiwango cha kutosha katika suala la usalama.
Kutokana na shambulio la magaidi
kwenye jengo la maduka,Westgate mjini Nairobi mwezi Septemba mwaka uliopita
Wakenya wengi wamepoteza imani juu ya idara za usalama. Lakini juu ya suala la
usalama Rais Uhuru Kenyatta amesema " usalama wa watu wetu na ulinzi wa
mipaka ya nchi ni miongomi mwa wajibu wangu mkuu." Rais Kenyatta amesema
vitisho vyovyote dhidi ya mipaka ya Kenya vitakabiliwa kwa uwezo na nguvu zote
za watu wa Kenya.
Umaarufu wa Kenyatta katika utaifa
Katika upande mwingine Rais Kenyatta
anatumia turufu ya utaifa ili kuhakikisha umaarufu wake. Hata kesi inayomkabili
kwenye Mahakama Kuu ya Kimataifa ya ICC inapalilia umaarufu wake.
Rais Kenyatta anakabiliwa mashkata ya
uhalifu dhidi ya binadamu. Katika ghasia zilizotokea nchini Kenya kufuatia
uchaguzi wa Rais mnamo mwaka wa 2007 inadaiwa kuwa Kenyatta ambae wakati huo
alikuwa kiongozi wa chama ndiye aliehamamisha makundi yaliyowatimua watu wa
makabila mengine,yaliyofanya ubakaji na kuwaandama watu wa jamii nyingine.
Mwandishi:Fischer ,Hilke,
Tafisiri:Mtullya Abdu.
Mhariri:Yusuf Saumu
DW.DE
No comments:
Post a Comment