Watu
watatu akiwamo Diwani wa Kata ya Mwendakulima ya Halmashauri
ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Ntabo Majhabi wanashikiliwa na polisi kwa
tuhuma za kufunga ofisi za serikali za mtendaji wa kata hiyo.
Wanadaiwa kutenda kosa hilo wiki
iliyopita asubuhi baada ya mtendaji wa
kata hiyo, Cecilia Clement kupigiwa simu
na mlinzi wa ofisi hizo, Joseph Katambi na kumpa taarifa za tukio hilo
liliofanywa na wananchi 15 walioambatana na diwani huyo.
Kwa mujibu mtendaji huyo, waliamua
kuibadilisha kamati ya sungusungu ya kata hiyo hali ambayo ilianza kuleta
malalamiko na minong’ono na kwamba huenda ni chanzo cha watuhumiwa hao kufunga
ofisi hizo.
Aliwataja wengine walikamatwa kuwa ni
fundi selemala,Hamisi Abbas na Makaka
Benedictor, wakazi wa kata hiyo.
Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Wilaya ya
Kahama, Benson Mpesya akiongozana na
kamati ya ulinzi ya kata na askari polisi, walifika katika ofisi hiyo kushuhudia mlango huo ulivyofungwa kwa
kuwekewa kipande cha bati na kupigiliwa misumari na mawe.
Mpesya alitoa amri ya kuvunjwa kwa bati hilo chini
ya ulinzi wa polisi na kuamuru waliohusika akiwamo diwani huyo kukamatwa na
kutiwa mbaroni.
Akizungumzia kitendo hicho Mpesya,
alisema ni fedheha na kisichoweza kuvumilika .
Chanzo: Ipp Media
No comments:
Post a Comment