Wawili hao waliuawa katika eneo la
Galkayo katika mpaka na Puntland
Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Nicholas Kay, ameshutumu mauaji ya washauri
wawili wa Umoja wa Mataifa ambao wamekuwa wakifanyakazi katika kitengo cha
Ofisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC).
Washauri hao wawili wa kimataifa
walikuwa Galkayo kusaidia jitihada za Ofisi ya UNODC katika eneo hilo wakati
walipouawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana katika uwanja wa ndege wa
Galkayo, Puntland, Somalia.
Umoja wa Mataifa umesema unawalaani
wauaji hao.
"Wafanyakazi wenzetu wa Umoja wa
Mataifa walikuwa wakifanyakazi ya kuwasaidia wananchi wa Somalia kufikia ndoto
yao ya kuwa na taifa lenye amani na imara. Hakuna uhalali wowote wa kufanyika
shambulio hilo.
Natoa wito kwa serikali kufanya
uchunguzi wa kina ili kuwabaini wahalifu hao na kuwafikisha kwenye vyombo vya
sheria bila kuchelewa".Amesema Bwana Kay.
"Natoa salamu zangu za pole kwa
familia na marafiki wa watu hao waliouawa.
Umoja wa Mataifa umedhamiria
kuendelea na msaada wao wa dhati kwa wananchi wa Somalia ambao wanatoka katika
mgogoro uliodumu kwa miongo kadhaa," amesema Mwakilishi huyo Maalum wa
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bwana Kay.
Habari kutoka Mohadishu, Somalia,
zinasema kikundi cha wapiganaji wa al-Shabab kimepongeza mauaji hayo na kudai
kufurahishwa na taarifa hizo za kuuawa kwa raia wa kigeni katika mji wa
Galkayo, katikati mwa Somalia Jumatatu.
"TUnapongeza na kufurahishwa na
mauaji ya maafisa wa Umoja wa Mataifa, leo. Mashirika ya Umoja wa Mataifa daima
ni maadui wa Waislam na Wasomali na vifo vyao vimelifurahisha kundi la
wapiganaji wa Mujahdeen" wamesema.
Walipoulizwa kama wanahusika na
mauaji hayo, al-Shabab wamesema kwa sasa hawapingi wala kudai kuhusika na
mauaji hayo”
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment