Akina mama wakiwa katika msururu wa kupiga kura mjini Kabul. (05.04.2014)
Rais Hamid Karzai akipiga kura yake mjini Kabul.(05.04.2014)
Msururu wa wapiga kura huko Mazar.(05.04.2014).
Rais Hamid Karzai akipiga kura yake mjini Kabul.(05.04.2014)
Msururu wa wapiga kura huko Mazar.(05.04.2014).
Mkongwe
akitumia haki yake ya kupiga kura Kabul.(05.04.2014).
Wananchi wa Afghanistan wamejitokeza
kwa wingi Jumamosi (05.04.2014) yakiwemo maeneo ya hatari kumchaguwa mtu wa
kuchukuwa nafasi ya Rais Hamid Karzai katika makabidhiano ya kwanza ya madaraka
kwa njia ya kidemkrasia.
Wananchi wa Afghanistan wamejitokeza
kwa wingi Jumamosi(05.04.2014) kumchaguwa mtu wa kuchukuwa nafasi ya Rais Hamid
Karzai katika makabidhiano ya kwanza ya madaraka kwa njia ya kidemokrasia
wakati vikosi vinavyoongozwa na Marekani vikikamilisha vita vyao vya miaka 13
nchini humo.
Licha ya vitisho vya kundi la Taliban
upigaji kura kwa kiasi kikubwa ulifanyika kwa amani huku kukiwa na misururu
mirefu katika miji nchini kote wakati wapiga kura wakipiga kura zao chini ya
ulinzi mkali takriban katika vituo 6,000.
Taliban imeukataa uchaguzi huo kuwa
ni njama ya kigeni na imewataka wapiganaji wake kushambuliwa wafanyakazi wa
uchaguzi,wapiga kura na vikosi vya usalama lakini hakuna shambulio lolote kubwa
lililorepotiwa wakati wa mchana.
Mkuu wa Tume Huru ya Uchaguzi (IEC)
Ahmad Yusuf Nuristani ameliambia shirika la habari la AFP kwamba watu wengi
wamejitokeza kupiga kura kuliko vile ilivyotarajiwa lakini hakutaja idadi bali
amesema idadi hiyo ni ndogo katika maeneo ya vijijini kulinganisha na mijini.
Ameongeza kusema kwamba wamepata
taarifa ya kupungukiwa na makaratasi ya kupiga kura na ameviagiza vituo vya
majimbo kutowa makatarasi zaidi ya kupigia kura.
Vituo vya kupigia kura vimeanza
kufungwa baada ya saa tano za kupiga kura, hapo awali ilitangazwa kwamba watu
walioko kwenye misururu ya kupia kura wataendelea kupiga kura zao.
Mjini Kabul ambapo kulikuwepo na
mfululizo wa mashambulio wakati yaliosababisha maafa wakati wa kampeni za
uchaguzi,mamia ya watu wamepiga misururu hadharani kupiga kura licha ya kuwepo
kwa mvua kubwa na ahadi ya waasi kuvuruga uchaguzi huo kwa matumizi ya nguvu.
Laila Neyazi mama wa nyumbani mwenye
umri wa miaka 48 amekaririwa akisema "Siogopi vitisho vya Taliban kwani
kwa vyo vyote vile iko siku tutakufa. Nataka kura yangu iwe muadhara kwa Taliban."
Usalama katika uchaguzi huo lilikuwa
suala lililozusha wasi wasi mkubwa kufuatia mashambulizi mjini Kabul likiwemo
la Jumatano lililouwa askari polisi sita.
Mashambulizi yasababisha maafa
Mkuu wa IEC Nuristani amesema
mashambulizi au hofu ya kuzuka matumizi ya nguvu vimelazimisha kutofunguliwa
kwa vituo 211 kati ya 6,423.
Siku moja kabla ya uchaguzi huu mpiga
picha wa shirika la habari la AP Anja Niedringhaus aliuwawa kwa kupigwa risasi
na kamanda mmoja wa polisi katika jimbo la mashariki la Khost.
Huyo ni mwandishi wa tatu
anayefanyakazi na vyombo vya habari vya kimataifa kuuwawa wakati wa kampeni za
uchaguzi baada ya kuuwawa kwa mwandishi habari wa Sweden Nils Horner na Sardar
Ahmad wa shirila la habari la AFP.
Waziri wa mambo ya ndani Omar Daudzai
amesema kikosi kizima cha Afghanistan cha askari 400,000 wa polisi,jeshi na
wanausalama wamewekwa kuhakikisha usalama nchini kote.
Waafghanistan wamechukuwa majukumu ya
usalama mwaka huu kutoka vikosi vinavyoongozwa na Marekani mwaka ambao ni wa
mwisho kwa vikosi vya muungano vya Jumuiya ya Kujihami ya NATO vya wanajeshi
51, 000 wa mapambano kuondoka nchini humo na kuwaachilia vikosi vya nchi hiyo
kupambana na uasi wa kundi la Taliban bila ya msaada wao.
Katika mji wa magharibi wa Herat
misururu ya mamia ya watu ilikuwa ikisubiri kupiga kura katika kituo kimoja cha
kupigia kura wakati huko Jalalabad mashariki mwa nchi hiyo wapigaji kura
walikuwa wakisubiri kwa uvumilivu nje ya msikiti mmoja.
Wapiga kura pia walikuwa katika
misururu katika mji wa Kandahar ngome ya Taliban kusini mwa nchi hiyo baadhi ya
wanawake wakiwa miongoni mwa wapiga kura kinyume na ilivyokuwa katika uchaguzi
wa mwaka 2009 ambapo idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura ilikuwa ndogo sana
kutokana na hali mbaya ya usalama.
Uchaguzi huu wa rais wa tatu nchini
humo unakamilisha miaka 13 ya utawala wa Karzai ambaye amekuwa madarakani tokea
Taliban walipopinduliwa hapo mwaka 2001.
Wagombea wakuu
Takriban watu milioni 13.5 wana haki
ya kupiga kura kutoka idadi ya watu wa nchi hiyo inayokadiriwa kufikia milioni
28.
Ziada ya duru hiyo ya kwanza ya
uchaguzi wa rais,wapiga kura pia wanayachaguwa mabaraza ya majimbo.
Wagombea walioko mstari wa mbele
kuwania nafasi inayoachwa na Karzai ni waziri mkuu wa zamani wa mambo ya nchi
za nje Zalmai Rassoul na Abdullah Abdullah ambaye alikuwa mshindi wa pili
katika uchaguzi mwa mwaka 2009 na mwanataaluma wa Benki ya Dunia Ashraf Ghani.
Hakuna anayewekewa matumaini makubwa
ya kushinda na iwapo hakuna mgombea atakayepata zaidi ya asilimia 50 ya kura
katika duru hiyo ya kwanza ambapo matokeo ya awali yanatarajiwa kutangazwa hapo
tarehe 24 mwezi wa Aprili,marudio yatafanyika mwishoni mwa mwezi wa Mei.
Udanganyifu mkubwa na matumizi ya
nguvu yaliozagaa yalitia dosari kuchaguliwa tena kwa Karzai hapo mwaka 2009 na
matokeo yatakayobishiwa safari hii yatazidi kuzidisha changamoto zinazomkabili
rais mpya.
Yoyote atakayeibuka mshindi itabidi
aongoze mapambano dhidi ya Taliban bila ya msaada zaidi wa vikosi vya Jumuiya
ya Kujihami ya NATO na pia kuimarisha kujitegemea kiuchumi kutokana na
kupunguwa kwa misaada ya fedha.
Uchaguzi huyo yumkini ukatowa fursa
kwa Afghanistan kuboresha uhusiano wake na Marekani ambayo ni mfadhili wake
mkuu baada ya miaka mingi ya kigeugeu cha Karzai.
Uhusiano huo ulizidi kudhoofika
mwishoni mwa mwaka jana wakati Karzai alipogoma kusaini makubaliano ya usalama
ambayo yangeliiruhusu Marekani kubakisha kama wanajeshi 10,000 nchini
Afghanistan kuwapatia mafunzo wanajeshi wa nchi hiyo na kuliandama kundi la Al
Qaeda.
Mwandishi :Mohamed Dahman/AFP/AP
Mhariri:Sekione Kitojo
No comments:
Post a Comment