Vyombo vya usalama nchini Afghanistan
viko katika hali ya tahadhari kuu baada siku moja tu kabla ya uchaguzi mkuu wa
urais katika taifa hilo lililosakamwa na vita.
Zaidi ya askari laki mbili wametumwa
kote nchini kulinda raiya dhidi ya mashambulizi ya taliban wakitekelza jukumu
lao la kikatiba ambalo kundi hilo la kislamu inapinga .
Tume huru ya uchaguzi ya afghanistan
imesema kuwa imekwisha wasilisha vifaa vya kupigia kura .
Msemaji wa wa tume hiyo Noor Mohammad
Noor, amesema kuwa maandalizi ya uchaguzi yamekamilika.
Wagombea urais wanachini ya saa 12
kukamilisha kampein zao tayari kwa uchaguzi huo utakaoandaliwa kesho.
Mshindi atatangazwa katika raundi ya
kwanza iwapo mgombea atasajili takriban asilimia hamsini ya kura zitakazopigwa
.
Mkondo wa pili utaandaliwa tu iwapo
hakutakuwa na mgombea atakayefikisha asilimia hamsini.
Rais anayeondoka Hamid Karzai hawezi
kugombea kwani amekwisha ongoza kwa vipindi viwili.
Viongozi 8 Wanagombea kumrithi rais
Karzai ambaye ameongoza tangu mwaka wa 2001 utawala wa Taliban ulipoondolewa
mamlakani.
Wagombea wakuu ni Abdullah Abdullah
na Zalmai Rassoul, ambao wamewahi kuhudumu kama mawaziri wa maswala ya Kigeni
na Ashraf Ghani Ahmadzai ambaye aliwahi kuhudumu kama waziri wa fedha.
No comments:
Post a Comment