Al Jazeera English journalists Peter Greste, Mohamed Fahmy, and Baher Mohamed have been held in jail in Egypt for 100 days.
Mashirika ya vyombo vya habari
yamerejelea wito wa kutaka kuachiliwa huru kwa waandishi watatu wa habari wa
shirika la al-Jazeera ambao wamekuwa wakishikiliwa kwa siku 100 sasa tangu
wakamatwe nchini Misri.
Waandishi hao watatu, akiwemo
mwandishi wa habari wa zamani wa BBC, Peter Greste, walifunguliwa mashitaka
mwezi Februari, wakituhumiwa kusambaza habari za uongo na kukisaidia kikundi
cha ugaidi.
Wamekana mashitaka hayo, ambayo
al-Jazeera imeyaita kuwa ni "upuuzi."
Kesi hiyo imechochea shutuma kutoka
vyombo vya habari vya kimataifa na makundi ya kutetea haki za binadamu duniani
kote.
Waandishi hao watatu ni miongoni mwa
watu 20 wanaokabiliwa na mashitaka kama yao. Ni watu wanane tu ambao mpaka sasa
wako gerezani, ambapo wengine 12 wamesomewa mashitaka bila kuwepo mahakamani.
Mwandishi wa nne wa al-Jazeera,
Abdullah al-Shami, ambaye anafanyia chaneli ya Kiarabu, anashikiliwa tangu
mwezi Agosti bila ya kufunguliwa mashitaka.
Bwana al-Shami amekuwa katika mgomo
wa kula na mke wake amesema afya yake inazorota.
Source: Al Jazeera
No comments:
Post a Comment