Milipuko mitatu katika mji mkuu wa
Kenya wa Nairobi imesababisha vifo vya watu 6 na karibu darzeni mbili
kujeruhiwa jumatatu usiku katika mtaa mkubwa wenye wakazi wengi wa asili ya
Kisomali wa Eastleigh.
Mkuu wa polisi wa County ya Nairobi
Benson Kibue anasema milipuko hiyo ilitokea takriban saa moja na nusu usiku na
kwa karibu wakati mmoja katika migahawa ya Sheraton Café na The New Kwa
muzairua Grill.
Kufuatana na mmiliki wa Sheraton Café
Bw. Patrick Gakuyu watu walikuwa wanatizama taarifa ya habari ya saa moja
kwenye televisheni wakati aliposikia milipuko miwili na umeme kuzimika na kuwa
katika kiza. Anasema anadhani ni grunetti mbili zilizorushwa ndani ya mgahawa
wake.
Jumapili usiku karibu na mtaa huo mtu
anayedhaniwa ni gaidi aliuwawa alipokuwa anatengeneza milipuko yake pamoja na
wenzake watatu. Na gruneti moja ilipatikana siku hiyo hiyo ya jumapili katika
mji wa pwani wa Lamu ndani ya kanisa moja.
Usalama umeimarishwa katika miji
mikuu ya Kenya na hadi hivi sasa haijulikani aliyehusika na mashambulio ya
jumatatu.
Chanzo: Mjengwablog
No comments:
Post a Comment