Watu waliokamatwa katika msako mjini Nairobi wakiingizwa uwanja wa mpira wa Kasarani
Serikali ya Kenya imesema kwa sasa
inawashikilia zaidi ya watu elfu nne kufuatia operesheni usalama nchini humo.
Msako huo wa kamatakamata ulianza
baada ya mashambulio ya magruneti wiki iliyopita katika eneo la Eastleigh
jijini Nairobi, ambalo wakaazi wake wengi ni wa jamii ya Kisomali.
Wengi wa watuhumiwa ni Wasomali.
Wengi wao wanashikiliwa kwa siku tatu
katika uwanja wa mpira wa Kasarani jijini Nairobi. Umoja wa Mataifa, makundi ya
kutetea haki na ndugu wa watu waliokamatwa wamesema wamenyimwa nafasi ya
kukutana na watuhumiwa hao.
Waziri wa mambo ya Ndani wa Kenya,
Joseph Ole Lenku, amesema wale ambao hawana vitambulisho kuhusu ukaazi au uraia
wao wa Kenya, watafikishwa mahakamani na huenda wakarejeshwa Somalia.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment