Idadi kubwa ya Wanatunduru huishi nyumba hizi sana maeneo ya vijijini. Idadi hiyo inakadiliwa kufikia zaidi ya asilimia 60.
HUU NI MJI MKONGWE WA TUNDURU, Picha ya Mwaka 2013
Wakazi wa Wilaya ya Tunduru wakiwa kwenye miangaiko ya Kila siku Wilayani hapo
Chiwambo's Blogu ilifika moja kwa moja hadi kituo kikuu cha kuuzia magazeti Eneo la Mwembe Riziki huko wilayani Tunduru na kujionea namna magazeti yanavyochelewa kuingia mjini hapo.
NA Ausi Chiwambo
Ni miaka mingi tangia nchi kuwa huru
wilaya hii kongwe nchini bado watu na wilaya yake i Maskini. Idadi kubwa ya
Wakazi wa wilaya ya Tutunduru mkoani Ruvuma hutegemea kilimo cha korosho na mpunga ile hali
teknologia ya kilimo hicho bado haijawafikia wakazi.
Pia katika mwamuko wa wananchi katika
masuala mbalimbali ya kimaendeleo ni mdogo kupita kiasi kwa sababu bado
wananchi hawaelimishwa vya kutosha katika kuandaa na kutunza miradi yao ya
kimaendeleo. Wananchi ni wagumu sana kuchangia masuala ya kimaendeleo hasa pale
inapotokea michongo ya kifedha na nguvu.
Baadhi ya wananchi wapo tayari
kufungwa lakini sio kuchangia miradi hiyo. Chiwambo's blogu ilitembelea baadhi
ya vijiji vilivyopo wilaya hiyo na kujionea namna wananchi wanavyokataa
kuchangia ili kupata miradi ya kimaendeleo. Mwandishi wa makala hii akizungumza
na wasomi mbalimbali wa Wilaya hiyo pia waliibua hoja ya baadhi ya Wananchi kuzuia
watoto wao kwa kuwaeleza kuwa wasifahuru mitihani yao ya kitaifa ili waweze
kuepukana na jela kwa madai kuwa hawana fedha za kuwasomeshea na wengine
huolewa au kuoa mara tu baada ya kumaliza elimu ya msingi.
Katika tafiti iliyofanywa na
Chiwambo's Blogu imebaini kuwa idadi ya Wanatunduru wanao ingia katika majukumu
ya kuwa Wazazi kabla ya Umri ni kubwa kupita kiasi hasa maeneo ya vijijini
ambako uelewa wa wananchi kuhusu masuala ya uzazi bado ni mdogo.
Ni matarajio yetu kuwa viongozi wa
wilaya ya Tunduru, Wasomi wa Wilaya hiyo, pamoja na Viongozi wa vijiji
watachukua hatua za haraka kutatua tatizo hilo kwa kuhamasisha wananchi kupitia
vikundi vyao kuelimishana na kuwapa moyo wa kuchangia miradi ya kimaendeleo.
0753-110740
No comments:
Post a Comment