Friday, April 4, 2014

Picha ya Rais Obama yazua kizaa zaa


                              Ortiz amekana madai ya kulipwa na kampuni ya Samsung kwa picha hiyo

Ikulu ya Whitehouse imeikashifu kampuni ya simu ya Samsung kwa kutumia picha ya Rais Barack Obama aliyojipiga na mchezaji maarufu nchini Marekani David Ortiz kama tangazo la kibiashara.
Picha hiyo ilipigwa na Ortiz mwenyewe akiwa na Rais Obama akitumia simu yake ya Samsung mapema wiki.

Hata hivyo kampuni ya Samsung iliisambaza kupitia kwa mtandao wa kijami wa Twitter kwa wateja wake na watu milioni 5.2 wanaoifuata kwa Twitter.
Msemaji wa Ikulu ya White House, Jay Carney, alisema kuwa picha ya Rais haipaswi kwa njia yoyote kutumiwa kwa sababu za kujinufaisha kibiashara.
Wakuu wa Samsung hawajasema lolote kuhusu malalamiko ya White House.

Ortiz mwenyewe alisema kuwa watu zaidi ya 40,00 waliisambaza picha hiyo kupitia Twitter

Bwana Carney amesema kuwa mawakili wa White House wanashauriwa kuhusu kitendo hicho cha Samsung.
"bila ya kusema mambo mengi, nataka niwaambie tu kwamba White House inapinga vikali jambo hili,'' alisema Carney

Ortiz alimpa Rais Obama Jezzi maalum kutoka kwa klabu anayochezea ya Red Sox ikiwa na jina la Rais siku ya Jumanne na jkisha kumshawishi kujipiga naye picha mwenyewe inayojulikana kama 'Selfie'.

"Nilimpa Jezzi na wapiga picha waka wanatupiga picha, basi nilijhisi na mimi kujipiga naye picha'' alisema mchezaji huyo.
Alikana kuwa kampuni ya Samsung ilimlipa pesa kwa picha hio.
Chanzo: BBC Swahili

No comments: