Mapigano yamezuka kati ya wabunge wa Ukraine mjini Kiev
Hali inatisha mashariki ya Ukraine
ambako wanaharakati wanaoelemea upande wa Urusi wamejitangazia "Jamhuri ya
Donetsk". Urusi imeonya dhidi ya hatari ya kuzuka vita vya wenyewe kwa
wenyewe Ukraine ikiingilia kati.
"Waasi wanaobeba
silaha,wanaopigania kujitenga maeneo ya mashariki,walioyavamia majengo ya
serikali wataandamwa kuambatana na katiba na sheria na kulinganishwa na magaidi
na wahalifu" amesema hayo rais wa mpito Olexandre Turtchinov.
Akihutubia bungeni hii leo rais
Turtchinov amesisitiza jeshi halitoshamiri silaha dhidi ya watu wanaoandamana
kwa amani katika wakati ambapo wanaharakati wanaoelemea upande wa Urusi
wanadhibiti majengo ya serikali maashariki ya nchi hiyo nayo Urusi inaonya
dhidi ya hatari ya kuripuka vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Rais Turtchinov
amethibitisha silaha na maguruneti yametumiwa dhidi ya vikosi vya wanajeshi
waliowekwa kulinda majengo ya serikali katika mji wa Kharkiv na kwamba
wanajeshi kadhaa wamejeruhiwa. Ameelezea matumaini yake kuyaona majengo ya
setrikali yakikombolewa haraka huko Lougansk na shughuli za tawala kuendelea
kama kawaida katika mji wa Donetsk ambako wanaharakati wanaoelemea upande wa
Urusi wametangaza "jamhuri yao".
Urusi imeitaka Ukraine iache
maandalizi ya kuingilia kijeshi katika maeneo hayo ya mashariki. Wizara ya
mambo ya nchi za nje ya Urusi inahoji watumishi wa shirika la kibinafsi la
Marekani wanashiriki katika opereshini hizo.
Jumuia ya Kimataifa itakutana Haraka
kuzungumzia Ukraine
Katika wakati ambapo Urusi inaonya
dhidi ya hatari ya kuzuka vita vya wenyewe kwa wenyewe katika maeneo ya
mashariki ya Ukraine,jumuia ya kujihami ya NATO imeitolea wito Moscow
iwarejeshe nyuma wanajeshi wake waliokusanywa karibu na mpaka wa nchi hizo
mbili.
Wakati huo huo waziri wa mambo ya
nchi za nje wa Marekani John Kerry amezungumza kwa simu na waziri mwwenzake wa
urusi Sergei Lavrov na kumuonya Washington inafuatilizia kwa wasi wasi mkubwa
yanayotokea Mashariki ya Ukraine.Waziri Kerry ameitaka Urusi ijitenganishe na
wanaopigania kujitenga eneo hilo,wanaofanya fujo na kuchochea mizozo.
Mawaziri hao wawili wamezungumzia
umuhimu wa kuitishwa mkutano kati ya Ukraine, Urusi, Marekani na Umoja wa Ulaya
ili kumaliza mivutano.
Bendera za Urusi zapepea Mashariki ya
Ukraine
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa
Ujerumani Frank-Walter Steinemeir anasema:"Tunabidi tufanye bidii
kuisaidia Ukraine kiuchumi na kisiasa. Juhudi hizo hazitafanikiwa mtengano
ukitokea nchini humo.
Yadhihirika kana kwamba hilo ndilo
linalotokea;bendera za Urusi zinapepea katika majrengo yote yanayokaliwa na
waasi mashariki ya Ukraine.
Mwandishi:Hamidou
Oummilkheir/AFP/Reuters
Mhariri: Josephat Charo
No comments:
Post a Comment