Majeneza ya wahanga wa mauwaji
Katika wakati ambapo Rwanda
inatafakari miaka 20 baada ya mauwaji ya halaiki, taasisi ya wanasheria ya
Ufaransa imefanikiwa kumhukumu mmojawapo wa waandalizi wa mauaji hayo ya
halaiki Pascal Simbikangwa.
Kesi ya kwanza ya mnyarwanda
aliyekuwa akituhumiwa kuhisika na mauwaji ya halaiki ni hatua muhimu kwa jopo
hilo maalum la mjini Paris linaloshughulikia masuala ya aina hiyo na ambalo
linaanza kupanua shughuli zake-anasema naibu mwendesha mashtaka mkuu Aurélia
Devos.
Pascal Simbikangwa,myarwanda wa
kwanza kuhukumiwa nchini Ufaransa kwa makosa ya kushiriki katika mauwaji ya
halaiki ya watu wa kabila la tutsi mnamo mwaka 1994,alihukumiwa kifungo cha
miaka 25 jela Marchi 15 iliyopita,na kuipatia jaza ya kwanza taasisi hiyo
inayoshughulikia masuala ya mauwaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya
ubinaadamumbele ya mahakama ya mjini Paris.
Ikiundwa mapema mwaka 2012,taasisi
hiyo imejiwekea lengo la kupambana dhidi ya mitindo ya kutoandamwa kisheria
wahalifu wa vita ambao wamekimbilia nchini Ufaransa nchi yenye idadi kubwa ya
wahamiaji.
"Ni hatua muhimu" amesema
Aurélia Devos ambae ni mkuu wa taasisi hiyo ya masuala ya sheria."Kesi
dhidi ya Pascal Simbikangwa imebainisha kwa mkumbo mmoja kwamba ni halali na ni
jambo linalowezekana kumfikisha mahakamani nchini Ufaransa mgeni yoyote,kwa
makosa aliyoyafanya katika pembe nyengine ya dunia."
Hata hivyo kesi hiyo ya kwanza sio
anzilishi,anahisi mwanasheria huyo na kusisitiza kwamba taasisi yake-mojawapo
ya mashirika madhubuti barani Ulaya,yenye majaji watatu,wanasheria wawili na wasaidizi
wao na wachunguzi 12 wanaokutana tangu mwezi wa februari katika ofisi yao
kuu,wanashughulikia masuala tofauti yanayopindukia yale yanayohusiana na
Rwanda.
Shabaha ni kurejesha uhusiano pamoja na Ufaransa
Kesi nyingi-27 kati ya 35
wanazozishughulikia zinawahusu watuhumiwa wa mauwaji ya halaiki ya Rwanda
waliohamia Ufaransa."Lakini nijuavyo mie haijawahi kuwa taasisi
inaoshughulikia suala la Rwanda tu" amehakikisha Aurélia Devos.Mashirika
kadhaa yamekuwa yakiituhumu taasisi hiyo tangu ilipoanzishwa kuwa chombo
kinachoshughulkia kutuliza uhusiano kati ya Paris na Kigali.
Mafuu ya wahanga wa mauwaji ya halaiki ya Rwanda
Uhusiano mbaya kati ya Ufaransa na
Rwanda ulikwenda umbali wa kuvunjwa uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo
mbili mwezi Novemba mwaka 2006.Uamuzi huo ulipitishwa baada ya jaji mmoja wa
kifaransa kutangaza waranti wa kukamatwa maafisa tisa wa Rwanda kuhusiana na
uchunguzi wa shambulio la April, sita mwaka 1994 lililopelekea kuuwawa rais wa
zamani wa kihutu Juvénal Habyarimana-chanzo cha kuzuka siku ya pili yake mauaji
ya halaiki nchini Rwanda.
Watuhumiwa wengine pia wanaandamwa
Katika wakati ambapo Pascal
Simbikangwa amehukumiwa kifungo cha miaka 25 jela,mnyarwanda mwengine Charkes
Twagira ametiwa korokoroni baada ya kukutikana na hatia ya kuhusika na mauwaji
ya halaiki na uhalifu dhidi ya ubinaadam.
Wanasheria wake wanatumia wakati
mwingi kutathmini hali ya isiasa,kihistoria,kiuchumi na kisaikolojia ya nchi
ambako uhalifu umetokea.Na kwa upande wa Rwanda mtu anaweza kusema ni kadhia
moja inayowahusu watuhumiwa 27.Anasema.Kadhia nyenginezo ambazo wanasheria wa
taasisi hiyo wanazishughulikia ni pamoja na ile ya Iraq, Libya,Tchad,Congo
Brazaville,jamhuri ya Afrika kati,Cambodjia na Maroko.
Pascal Simbikangwa ahukumiwa kifungo cha miaka 25 jela nchini Ufaransa
Na kadha nyengine kadhaa zinazohitaji
uchunguzi wa awali.Mojawapo ya kadhia hizo inahusu biashara ya zana za ukaguzi
iliyofanywa na kampuni ya Ufaransa Amesys kwa utawala wa zamani wa Muammar
Gaddafi nchini Libya-kampuni inayotuhumiwa na mashirika yasiyomilikiwa na
serikali,kusaidia katika kuwatesa wapinzani wa serikali.
"Hatujaribu kupanua uwanja wa
shughuli zetu-zipo tayari,anasisitiza mwanasheria huyo Aurélia Davos. Uwaja huo
umepata nguvu kutokana na kuongezeka vusa vya uhalifu dhidi ya ubinaadam.
Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Reuters
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman
No comments:
Post a Comment