Wanajeshi wa Chad walikwenda Bangui kusaidia wanajeshi wa Muungano wa Afrika kushika doria
Chad imeamua kuondoa wanajeshi wake
kutoka katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
Wanajeshi hao wamekuwa nchini humo
kwa miaka mingi.
Zaidi ya wanajeshi 850 wamekuwa
wakisaidia kikosi cha muungano wa Afrika kinachoshika doria nchini humo.
Lakini wamekosolewa kwa kuunga mkono
waasi wa kundi la kiisilamu la Seleka.
Waziri wa mambo ya nje wa Chad
amesema kuwa licha ya wanajeshi wake kujitolea kusaidia hali nchini CAR,
wamekuwa wakituhumiwa kwa kupendelea upande mmoja na kuchochea hali nchini
humo.
Taifa hilo la Magharibi mwa Afrika
limekumbwa na mgogoro wa kidini tangu waasi kuchukua mamlaka mwaka jana. Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment