Serikali ya Somalia inasema
imewakamata makamanda wawili waandamizi wa kundi la al-Shabab, mmoja wao ni
mshukiwa katika bomu ambalo liliuwa zaidi ya watu 20.
Maafisa waliwaonyesha wanaume hao wawili kwa waandishi wa habari
jumatatu katika mji wa Qoryoley lakini hawakuyataja majina yao wakielezea kile
kwamba ni kusubiriwa uchunguzi zaidi.
Naibu waziri wa usalama Ibrahim Isak
Yarrow anaiambia Sauti ya Amerika-VOA, Idhaa ya Kisomali kwamba mtu mmoja
anashukiwa kuwa alihusika katika shambulizi la Septemba mwaka 2009 la bomu la
kujitoa mhanga kwenye kituo cha walinda amani wa Umoja wa Afrika mjini Mogadishu.
Shambulizi liliuwa watu 21, watu 17
kati yao ni wanajeshi wa Afrika akiwemo naibu kamanda wa jeshi, Juvenal
Niyonguruza kutoka Burundi.
Mtu mwingine aliyekamatwa inasemekana
kuwa anatoa mafunzo kwa Amniyat,
kitengo cha ngazi ya juu katika kundi la
al-Shabab kinachohusika na operesheni za kujitoa mhanga, ujasusi na mauaji.
Vyanzo vinaiambia VOA kwamba
operesheni ya kuwakamata watu hao ilifanywa na kitengo maalumu kijulikanacho
kama Gaashan au Shield ambacho kilipatiwa mafunzo kwa msaada wa Marekani.
Chanzo: VOA
No comments:
Post a Comment