AZAM FC inahaha kila kona kuhakikisha
beki Shomari Kapombe anatua katika himaya yao tayari kwa ajili ya kumtumia
katika msimu ujao na imeweka mezani ofa ya maana kumnunua beki huyo kutoka AS
Cannes ya Ufaransa.
Akizungumza na Mwanaspoti kutoka
Ufaransa asubuhi jana (Ijumaa), wakala wa beki huyo Dennis Kadito alisema, Azam
imekuwa katika jitihada kubwa za kuhakikisha inamsajili mteja wake huyo, ambapo
awali kupitia kwa Yusuf Bakhresa walituma ofa ya Euro 40,000 (Sh milioni 88)
ambazo ziligomewa na Wafaransa hao.
Kadito alisema Cannes baada ya kugoma, Azam
waliwatajia kiasi ambacho wanakihitaji ili kumuuza beki huyo ambacho ni Euro
70,000 (Sh milioni 154) na Yusuf ambaye pia ni wakala wa kuuza wachezaji
alikubali kulipa.
Inadawa kwamba, Azam walikubali
kulipa kiasi hicho baada ya kugundua wameshafanya makosa ya kumshawishi Kapombe
avunje mkataba wake na Cannes na beki huyo tayari ameshawasilisha barua ya
kufanya hivyo tangu Februari 27, mwaka huu.
“Nilipigiwa simu na Yusuf ambaye
alitaka kumnunua Kapombe ili asajiliwe Azam FC kwa kiasi hicho cha Euro elfu 40
lakini kikakataliwa na Cannes ambako wanataka elfu 70,Yusuf hakukubali akasema
ataangalia jinsi ya kutumia sheria kumpata Kapombe.
“Baadaye Kapombe alituma barua Cannes
akitaka mkataba wake na klabu hiyo uvunjwe, barua hiyo iliandikwa na mchezaji
mwenyewe lakini ukiichunguza kwa makini ni wazi kwamba alipata msaada kutoka
kwa wanasheria,” aliongeza Kadito licha ya kwamba Yusuf hakupatikana jana kutoa
ufafanuzi wa suala hilo.
Chanzo: Mwanaspoti
No comments:
Post a Comment