Bunge kufichua siri za CIA
Kamati ya bunge la Marekani kuhusu
ujasusi imeidhinisha kuwekwa wazi kwa sehemu mojawepo ya ripoti iliyoiita ya
"ukatili" ilioelezea jinsi maafisa wa shiriki la upelelezi la
Marekani CIA linavyowahoji wanatuhumiwa wa ugaidi.
Lakini wanakamati wanasema kuwa
itachukua muda kabla ya uchunguzi huo kuwekwa wazi kwa umma.
Sehemu ya ripoti iliyofichuliwa
inasema kuwa idara ya CIA kila mara ilipotosha serikali kuhusiana na mtindo
wake wa kuhoji washukiwa wa ugaidi wakati wa utawala wa Rais George W Bush.
CIA inapinga baadhi ya matokeo ya
taarifa hiyo huku ikikiri kutenda matendo ambayo hayakuafikiana na sera za
Marekani.
Mwenyekiti wa kamati hiyo ya baraza
la Senate Dianne Feinstein anasema matokeo ya kura iliyopigwa kuhusu ripoti
hiyo inaonesha wabunge 11-3 waliipigia mswada huo kura huku akisema ni
uchunguzi wa matokeo yanayotamausha.
Stakabdhi za CIA Kufichuliwa kwa umma
"ripoti hiyo inaonyesha dhuluma
inayoenda kinyume na hadhi ya taifa letu,''alisema Dianne
Hii inatia doa historia ya taifa letu
na ambayo hairuhusiwi kamwe kufanyika. ''Hivi sivyo wamarekani wanavyofaa
kufanya." Mwanasiasa huyo wa chama cha Democrat kutoka Carlifonia amesema.
Taarifa ya wanahabari inasema kuwa
japo baadhi ya wanakamati wa chama cha Republican walikashifu ripoti hiyo kwa
pamoja na wa Democrats, kulionyesha waziwazi mgawanyiko uliopo ndani ya wajumbe
hao.
Matokeo ya uchunguzi huo uliyomo
katika kijitabu cha ukurasa 500, yatatumwa kwa Rais Barack Obama ili
kuchunguzwa, kutiwa saini, kisha kutolewa kwa umma.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment