Vikosi maalum vya Ukraine vikiwatuimua waasi huko Kharkiv
Waandamanaji wanaopigania kujiunga na Urusi mashariki ya Ukraine
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry na mwenzake wa Urusi Sergey Lavrov walipokutana Paris Marchi 30 iliyopita
Waandamanaji wanaopigania kujiunga na Urusi mashariki ya Ukraine
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry na mwenzake wa Urusi Sergey Lavrov walipokutana Paris Marchi 30 iliyopita
Polisi ya Ukraine imewatimuwa
wanamgambo wanaoelemea upande wa Urusi huko Kharkiv, lakini wanamgambo wenzao
wanaendelea kuyakalia majengo ya serikali huko Donetsk na Luhansk.
Ukraine ikiungwa mkono na Marekani na
nchi za Umoja wa ulaya inaituhumu Urusi kusimamia machafuko katika eneo la
mashariki na kuyarejea yale yale yaliyopelekea Moscow kuimeza raasi ya Crimea
mapema mwezi uliopita.Kama ilivyotokea Crimea,waandamanaji wameyavamia majengo
ya serikali jumapili usiku huko Kharkiv,Donetsk na Luhansk wakishinikiza kura
ya maoni iitishwe.
Urusi iliyokusanya wanajeshi wake
karibu na mpaka wa Ukraine imewaonya viongozi wepya wa mjini Kiev wasipuuze
madai ya majimbo yenye wakaazi wengi wanaozungumza kirusi-kusini mashariki ya
Ukraine, kitovu cha viwanda na migodi ya Ukraine.
Waziri wa ndani wa Ukraine Arsene
Avakov amesema wanamgambo wanaoelemea upande wa Urusi wametimuliwa Kharkiv
katika opereshini ya kupambana na magaidi iliyodumu dakika 18.
Waziri wa ndani Arsene Avakov
amewatwika rais Vladimir Putin wa Urusi na rais wa zamani wa Ukraine Viktor
Yanukovich jukumu la kukaliwa majengo hayo.
Urusi yalaumiwa kuwa nyuma ya uasi
huo
Wanamgambo 70 waliokamatwa
wanatuhumiwa na serikali ya Ukraine miongoni mwa mengineyo kuhusika na
"harakati haramu za uasi,kuchochea fujo miongoni mwa jamii na kusababisha
madhara kwa afya ya binaadam.
Hata hivyo waasi wanaendelea
kuyashikilia majengo ya serikali huko Donatsk na Luhansk ambako walivunja jengo
la idara ya upelelezi na kunyakuwa silaha.
Hali mashariki ya Ukraine inaangaliwa
kwa jicho la wasi wasi na nchi za magharibi,zinazohofia Urusi isije ikaitumia
biashara ya gesi kama turufu dhidi ya nchi za Umoja wa ulaya.
Marekani imeionya Urusi isiingilie
kichini chini katika mzozo wa mashariki ya Ukraine ambako kwa maoni ya ikulu ya
Marekani kuna ishara za kuaminika zinazoonyesha wanamgambo wa Ukraine wanalipwa
ili wafanye fujo.
Msemaji wa uikulu ya Marekani Jay
Carney anasema:"Ikiwa Urusi itaingia mashariki ya Ukraine naiwe moja kwa
moja au kichini chini, hali ya mambo itazidi kuwa mbaya.Tunamtolea wito rais
Putin na serikali yake waache kuchochea vurugu nchini Ukraine.Na
tunawatahadharisha pia dhidi ya kuingilia kijeshi."
Katibu mkuu wa jumuia ya kujihami ya
NATO Anders Fogh Rasmussen nae pia ameionya Urusi akisema itafanya "kosa
la kihistoria" ikiamua kuivamia tena Ukraine.
Ishara njema yaanza kuchomoza
Ishara pekee ya kutulia hali ya
mambo,waziri Serguei Lavrov amethibitisha mkutano wa pande nne utakaozileta
pamoja Urusi,Marekani,Ukraine na umoja wa ulaya huenda ukaitishwa haraka kusaka
ufumbuzi wa mzozo wa Ukraine.
Mwandishi:Hamidou
Oummilkheir/Reuters/AFP/AP
Mhariri: Josephat Charo
No comments:
Post a Comment