Wazazi katika kaunti ya Kirinyaga
mkoa wa Kati nchini Kenya wameandamana kwa hasira baada ya mwalimu kumchapa
mtoto mmoja wa shule ya msingi hadi akafariki.
Mtoto huyo inaarifiwa alichapwa
kichwani na mwalimu na kuzirai. Alifariki alipokuwa anapelekwa hospitalini.
Wazazi hao waliandamana kwa amani
wakitaka hatua kali kuchukuliwa dhidi ya mwalimu huyo.
Hata hivyo polisi waliweza kumkamata
mwalimu huyo na kumpeleka kituoni huku uchunguzi ukianza kufanywa.
Mtoto huyo alikuwa katika darasa la
saba katika shule ya kibinafsi ya Roka Preparatory.
Inaarifiwa alizirai baada ya mwalimu
kumchapa kwenye kisogo.
Wazazi hao waliokuwa wanalalamikia
kile wanachosema ni wanafunzi kuadhibiwa vikali kwa makosa madogomadogo
walitaka mwalimu huyo achukuliwa hatua kali kwa kitendo hicho cha kumchapa
mwanafunzi ambacho kimeharamishwa katika shule zote nchini Kenya.
Wengi wa wazazi wenye watoto wao
katika shule hiyo wameahidi kuwahamishia shule nyingine.
Kenya iliharamisha kitendo cha
kuwachapa wanafunzi wa shule karibu miaka kumi iliyopita. Ilikuwa baada ya visa
vya walimu kuwaadhibu vikali wanafunzi na kuwajeruhi kukithiri.Chanzo: BBC
Swahili
No comments:
Post a Comment