Maafisa wa Polisi nchini Kenya
wanasema wamekamata zaidi ya watu elfu tatu katika msako dhidi ya wageni nchini
humo .
Msako huo ulianza Ijumaa, baada ya
mashambulizi ya gurunade wiki iliyopita katika eneo la Eastleigh linalokaliwa
zaidi na wasomali katika mji mkuu Nairobi.
Wengi wa waliokamatwa ni wasomali .
Inspekta mkuu wa polisi , David
Kimaiyo, amesema kuwa watu 450 bado korokoroni asili mia kubwa yao ikiwa katika
uwanja wa michezo wa Kasarani huku waliosalia wakiruhusiwa kwenda zao baada ya
kuchunguzwa na maafisa
wa usalama na wale wa uhamiaji
kubaini uhalali wao .
Umoja wa Mataifa, makundi ya kutetea
haki za binadamu na jamaa wa watu hao wanasema hawajapewa ruhusa ya kuwaona
wapendwa wao.
Waziri wa mambo ya ndani wa Kenya
Joseph Ole Lenku, anasema wale ambao hawana vibali vya kuishi nchini
watachukulia hatua zaidi.
Sitini na tisa wamepelekwa mahakamani
kwa madai ya kuwepo nchini Kenya bila idhini au kumiliki stakabadhi gushi.
Mwandishi wetu Robert Kiptoo ambaye
amezuru mtaa huo wa Eastleigh ametueleza kuwa msako wa polisi dhidi ya
wahamiaji haramu na washukiwa wa ugaidi bado unaendelea .
Msemaji wa polisi nchini Kenya Masoud
Mwinyi amekanusha madai kuwa polisi wanalenga jamii moja ama watu wa dini moja.
Mashirika ya kijamii na yale ya
kutetea haki za kibinadamu yanalalamika kuwa yamenyimwa fursa ya kuwatembelewa
washukiwa hao waliokamatwa.
Miongoni mwa waliokamatwa ni raia wa
Kenya, Uganda, Sudan, Sudan Kusini ,hata hivyo idadi kubwa inatoka Somalia.
Aidha ripoti zinasema kuwa wageni
wengi wamekimbilia miji mingine nchini Kenya kukwepa msako huo wa polisi
lakini.
Serikali imetoa onyo kwa Wakenya
kutowasaidi watu ambao wanawashuku kuwa wageni.
Serikali ya Kenya imeonya kuwa
haitawavulimia wakimbizi mijini ikisema kuwepo kwao mijini kunahujumu usalama
wa taifa.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment