Urusi imewakamata raiya 25 kutoka
Ukraine
Kitengo cha kimataifa cha upelelezi
Nchini Urusi FSB, kinasema kuwa kimewazuilia raia 25 wa Ukraine, kikiwalaumu
kwa kupanga mashambulio ya kigaidi mwezi uliopita wakati jimbo la
Crimea lililoko Ukraine lilipokuwa
likiandaa kura ya maoni.
Idara hiyo inasema watu hao
wanaozuiliwa walikuwa wanachama wa vuguvugu la ultra-nationalist na walikuwa
wakijiandaa kusababisha mashambulio hayo katikati na Kusini mwa Urusi.
Kikosi cha polisi cha Berkut
chalaumiwa kwa vifo wakati wa maandamano
Awali, waziri wa usalama wa taifa wa
Ukraine, Arsen Avakov amesema kuwa tume rasmi ya uchunguzi inaonyesha kuwa
kitengo maalum cha polisi kiitwacho Berkut kilichobuniwa kukabiliana na vurumai
kiliwauwa waandamanaji kadhaa katika uwanja wa maandamano mjini Kiev, mwezi
Februari.
Amesema kikosi hicho maalum cha
polisi kimevunjiliwa mbali.
Kaimu Waziri mkuu Arseniy Yatsenyuk
ameiambia BBC kuwa rais aliyeng'olewa madarakani Viktor Yanukovych na washirika
wake ndio wahusika wakuu katika maafa hayo.
Zaidi ya watu 100 waliuwawa katika
vurumai hilo.
Naye kiongozi mkuu wa upelelezi
Nchini Ukrainne Valentyn Nalyvaychenko amesema kuwa idara ya upelelezi ya Urusi
imetuma tani kadhaa za villipuzi na silaha hadi Ukraine.
Chanzo: BC Swahili
No comments:
Post a Comment