BARAZA la Habari Tanzania (MCT)
limetangaza majina saba ya wajumbe wapya wa jopo la wajuzi wa uhuru wa habari
wa kujiendeleza.
Majina hayo yalitangazwa mjini Dodoma
jana na Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga.
Katibu huyo aliwataja walioingia
kwenye jopo hilo kuwa ni Profesa Penina Mlama, Jenerali wa Ulimwengu, Profesa
Ruth Meena, Alli Ahmed Uki, Bonaventura Rutimwa, Ndimara Tegambwage na Wangethi
Mwangi.
“Jopo hili limechaguliwa kutokana na
vigezo vya kuleta tija, ujuzi na kuibua masuala mapya ya kuipeleka mbele
tasnia habari,” alisema huku akiongeza
kwamba huteuliwa kila baada ya miaka
mitatu.
Mukajanga aliwataja wajumbe waliopita
kuwa ni Profesa Issa Shivji, Profesa Robert White, Profesa Palamagamba Kabudi,
Profesa Penina, Saida Yahya, Wangethi, Ulimwengu na Dk. Peter Mwesige.
Wakati huohuo, alizungumzia
kuhusu mchakato wa Katiba mpya na
kuwataka Watanzania kuondoa hofu kutokana na kelele zinatokea ndani ya Bunge
Maalumu la Katiba, kwa kuwa ndiko kutakakosaidia kupatikana kwa katiba bora.
Aliwataka baadhi ya wajumbe wa Bunge
hilo kuacha kuleta masuala ya kisiasa katika Bunge hilo, kwa sababu ni la
maridhiano.
No comments:
Post a Comment