Nyumba ya Zuma iliyokarabatiwa
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma
amesema hadhani ni sawa kurejesha fedha za umma zilizotumiwa kukarabati nyumba
yake binafsi kwa sababu hakuwahi kutoa pendekezo hilo.
Bw. Zumaamesema haoni haja ya
kuchangia pesa zake binafsi katia ukarabati wa nyumba hiyo kwani halikuwa
pendekezo lake toka mwanzoni.
Kadhalika bwana Zuma ameambia runinga
moja nchini Afrika Kusini kwamba maafisa wa serikali ndio waliopanga ukarabati
huo uliogharimu dola milioni 23 bila kumuarifu.
Hii ndio mara ya kwanza Rais Zuma
amezungumzia kuhusu makaazi hayo yaliyozua mjadala mkali wa umma Afrika Kusini.
Mhifadhi wa mali ya umma alisema
baadhi ya ukarabati uliofanywa sio halali na kumtaka Zuma kurejesha baadhi ya
fedha zilizotumika.
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment