Wednesday, April 9, 2014

SHANGAZI WA RAIS OBAMA AFARIKI DUNIA.

Shangazi wa rais Obama  Zeituni  Onyango ambaye  kwa wakati fulani alinyimwa hifadhi hapa Marekani lakini akaendelea kuishi kinyume cha sheria kwa miaka kadhaa katika jimbo la Masachussets  amefariki  dunia akiwa na umri wa miaka 61.

Wakili wa masuala ya Uhamiaji wa  Onyango amesema amefariki katika hospitali moja baada ya kuugua ugonjwa saratani na matatizo ya kupumua . Aliugua tangu mwezi January.
Onyango alihamia Marekani kutoka Kenya mwaka 2000 na alinyimwa hifadhi ya kisiasa na jaji wa Uhamiaji mwaka 2004. Hakuondoka nchini na aliendelea kuishi kwenye nyumba za umma huko Boston. Hali yake ya ukaazi wa Marekani  ilitangazwa hadharani  siku chache kabla ya Bw.Obama kuchaguliwa rais Novemba 2008.


Chanzo: VOA

No comments: