WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro
Nyalandu, amewataka wafanyakazi wa wizara hiyo kuhakikisha wanatumia kila mwanya
uliopo kisheria kufanikisha mapambano dhidi ya vitendo vya ujangili.
Alitoa kauli hiyo mjini Morogoro jana
wakati akifungua baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo, na kusema vitendo vya
ujangili vimekuwa vikiathiri taswira ya maliasili, na kwamba hali hiyo
itabadilika iwapo wafanyakazi wenyewe watawajibika ipasavyo.
Aliwataka wafanyakazi hao kubadilisha
mwelekeo wa wizara hiyo na kupandisha morali ya kazi, kwani wizara ina
rasilimali nyingi zinazoweza kuliingizia pato taifa kwa asilimia 70.
Alisema pamoja na serikali kuwa na
mkakati wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), amewaasa watendaji wa wizara hiyo
kujiwekea mikakati yao wenyewe kiwizara, ili kufanya kazi kwa tija.
Alisema kuanzia Mei mwaka huu hadi
Julai, wizara itaanza kutoa mafunzo maalumu ya kupambana na ujangili kwa
kutumia helikopta.
Chanzo: Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment