Tuesday, November 5, 2013

WALIOMPIGA DKT. MVUNGI MBARONI




Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linawashikilia watu sita kwa tuhuma za kuhusika na tukio la kumvamia, kumjeruhi vibaya kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili hasa kichwani, Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dkt. Sengondo Mvungi.

Dkt.Mvungi ambaye pia ni Mjumbe wa Ha lmashauri Kuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi, amelazwa katika Chumba cha Wagonjwa Wana ohitaji Uangalizi Maalumu (ICU),kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), akiwa ha jitambui.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, alisema Dkt. Mvungi alivamiwa nyumbani kwake Novemba 3 mw aka huu, Mpigi Magohe , mpakani mwa Mkoa wa DaresSalaam na Pwani.

Alisema katika tukio hilo watuhumiwa waliiba kompyuta mpakato moja aina ya HP,simu mbili za mkononi pamoja na pesa taslimu sh.milioni moja.
“Baada ya tukio polisi walianza ms ako mkali kwa kushirikiana na raia , tulifanikiwa kuwakamata watuhumiwa na baada ya kupekuliwa walikutwa na dawa za kulevya aina ya bhangi puli 17 pamoja na gongo lita 15,”alisema.
Aliongeza kuwa,jeshi hilo bado linaendelea n a msako ili kuwabaini watuhumiwa wengine.

James Mbatia azungumza
Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo,Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Taifa, Bw.James Mbatia, alisema hali ya Dkt. Mvungi imeanza kuimarika lakini bado hajaanza kupataf ahamu.

“Leo hali yake inatia matumaini tofauti na alivyoletwa,kama ataendelea hivi mambo yatakuwa mazuri zaidi,”alisema.
Aliongeza kuwa,leo familia yake itafanya misa ya kumuombea Dkt.Mvungi ili apate nafuu ambayo itafanyika katika Kanisa la St.Joseph , P osta Dar es Salaam, kuanzia saa 10 jioni .

“Nawashukuru Watanzania wote wakiwemo Mashekhe na Wanazuoni wa Kiislamu kwa kuja kumuona, kumuombea ili aweze kupona haraka,” alisema Bw. Mbatia.
Naye Msemaji wa Taasisi ya Mifupa(MOI ), Bw. Jumaa Almas, alisema Dkt.Mvungi anae ndelea vizuri tofauti na alivyokuja.
“Madaktari wanaendelea kumpa matibabu lakini hadi sasa, bado hajapata fahamu,yupo katika chumba cha uangalizi maalumu alisema Bw. Almas

No comments: