Thursday, November 7, 2013

Wakuu wa Kakao wafungwa jela Ivory Coast



Ivory Coast ndio inazalisha kiwango kikubwa zaidi cha Kakao duniani
Mahakama nchini Ivory Coast imewafunga jela watu 15 waliokuwa maafisa wakuu watendaji katika sekta ya Kahawa na Kakao nchini humo.
Maafisa hao walikuwa wanafanya kazi katika baraza la serikali la kudhibiti mauzo ya Kakao na kahawa na kila mmoja amefungwa jela miaka ishirini.

Maafisa wengine 15 waliachiliwa kwa kutopatikana na hatia mjini Abidjan.
Washitakiwa wanaojulikana kama wakuu wa biashara za Kakao, pia waliamrishwa kulipa faini ya hadi dola milioni lakini moja na arobaini.
Wamepatikana na hatia ya kufuja viwango vikubwa vya pesa za serikali zilizotokana na mapato ya kodi.

Maafisa hao walikamatwa mwaka 2008 baada ya aliyekuwa rais Laurent Gbagbo kuamuru uchunguzi kufanywa kutokana na madai ya ufisadi katika sekta ya Kahawa na Kakao.
Gbagbo alishindwa katika uchaguzi wa mwaka 2010 lakini akakataa kukubali matokeo hadi alipoondolewa mamlakani na wanajeshi watiifu kwa rais wa sasa Alassane Ouatarra manmo mwaka 2011.

Gbagbo sasa yuko katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu akisubiri kuanza kwa kesi yake ambapo anatuhumiwa kwa kosa la uhalifu dhidi ya binadamu. Gbagbo amekanusha madai hayo.
Ivory Coast ndio ndhi inayozalisha kiwango kikubwa zaidi cha kakao , ingawa sekta hiyo imedumaa kwa miaka mingo kutokana na mgogoro wa kisiasa wa miaka mingi nchini humo.
Chanzo: BBCSwahili

No comments: