Tuesday, November 5, 2013

Wawakilishi waongezewa posho

Zanzibar.Wakati wabunge wakitaka posho ya vikao iongozwe kutoka Sh100,000 hadi Sh300,000 kwa siku, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imepandisha posho kutoka Sh100,000 hadi 150,000 kuanzia mwaka huu.

Uchunguzi wa Mwananchi umebaini viwango hivyo vya posho vimeanza kutumika tangu kupitishwa kwa bajeti ya mwaka 2013/14, kila mjumbe analipwa kiwango hicho cha posho licha ya mshahara wake.
Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW), Yahya Khamis Hamad alithibitisha viwango hivyo vipya vya posho kuanza kutumia mbali na mishahara yao na posho mbalimbali za jimbo kila mwezi.

Hamad alisema nyongeza hiyo ya kikao imetokana na mapendekezo ya Kamati ya Uongozi ya BLW, baadaye kuridhiwa na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein.
Alisema kutokana na kupanda kwa gharama za maisha, kamati ya uongozi ina wajibu wa kuangalia kila mwaka maslahi ya wawakilishi, lakini mwaka jana posho za vikao hazikuangaliwa badala yake ziliangaliwa posho nyingine na mishahara yao.
Mabadiliko ya posho ya vikao mishara na posho mbalimbali za wajumbe yalifanyika mwaka 2012/13, kutoka Sh3.5 milioni hadi Sh4.5 milioni.
Chanzo: Mwananchi

No comments: