Sunday, November 3, 2013

Kilango awashambulia mawaziri




na Danson Kaijage, Dodoma
MBUNGE wa Same Mashariki, Anne Kilango (CCM), amewashambulia baadhi ya mawaziri wanaokaa vikaoni kupika majungu na kuwakwamisha mawaziri na wabunge wachapaka kazi.
Kilango alitoa kauli hiyo juzi alipokuwa akichangia mjadala wa Kamati ya Mipango ya Taifa ya mwaka 2014/16.

Kilango alisema taifa haliwezi kuwa na maendeleo na kamwe mipango haiwezi kukamilika kama baadhi ya mawaziri na wabunge wazembe wanakaa vikao kwa ajili ya kuwadhoofisa mawazri na wabunge wachapa kazi.
Kilango alisema serikali imekuwa na baadhi ya watumishi ambao kazi yao ni kupika majungu dhidi ya watumishi wachapa kazi.

Mbunge huyo alisema Watanzania wanatakiwa kutambua kuwa baadhi ya wanasiasa si wachapa kazi na badala yake wanakaa bungeni kwa ajili ya kuwalaumu wengine.
Alisema inasikitisha kuona Tanzania inakuwa na mipango mingi lakini haitekelezeki na zipo nchi nyingi ambazo zinakuja kujifunza mipango nchini na zinafanikiwa lakini Tanzania inaendelea kuwa maskini.

Kwa upange wake Mbunge wa Viti Maalumu, Cecilia Pareso (CHADEMA) alisema serikali bado inashindwa kutekeleza mipango yake kutokana na kuwa na mipango mingi ambayo haitekelezeki.
Pareso alitoa sababu nyingine ya kushindwa kwa mpango huo kuwa ni kutokana na bajeti ya serikali kuwa tegemezi.

Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Felister Bura (CCM), alisema kuwa anachoshwa na serikali kuwa na mpango wa kuhamia Dodoma lakini mpango huo upo katika makaratasi tu.
Chanzo: Tanzania Daima

No comments: