Tuesday, November 5, 2013

SUMAYE ‘KUTEMA CHECHE’ LEO




Waziri Mkuu mstaafu wa Awamu ya Tatu, Bw. Frederick Sumaye, leo anatarajia kuzungumza na waandishi wa habari pamoja na kutoa tamko la kumuunga mkono Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) ,Rais Jakaya Kikwete kwa kauli yake ya kukemea rushwa ndani ya chama hicho hasa kwa watu wanaotafuta madaraka.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kinasema kuwa, Bw. Sumaye atatoa tamko hilo leo saa tatu asubuhi katika Hoteli ya Court Yard iliyopo Upanga, Dar es Salaam.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa, pamoja na kuto a tamko hilo pia atazungumzia tukio la hivi karibuni akidaiwa kuhujumiwa mwaliko aliopewa na vijana wa asasi ya kuelimisha jamii kuhusu usalama na amani (Public Ter rorism Awareness Trust Fund and Human Welfare(PTA-HW).

Asasi hiyo iliandaa tamasha ambalo lilipa ngwa kufanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja,Dar es Salaam na kumwalika Bw. Sumaye kuwa mgeni rasmi lakini katika mazingira ya kutatanisha , saa chache kabla ya shu ghuli hiyo aliambiwa imeahirishwa na atataarifiwa tarehe nyingine itakayopangwa.

Katika hali isiyo ya kawaida, maandamano ya vij ana hao yaliwasili katika viwanja hivyo ambapo Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), kutoka Wilaya ya Bukoba Vijijini, mkoani Kagera, Bw. Naziri Karamagi, aliyapokea maandamano hayo.
Dalili za mgawanyiko miongoni mwa waandaaji,zilijitokeza baadaya kuwasili kwa Bw.Karamagi ambaye hakuwa ametarajiwa na waandaaji pamoja na washiriki wa tamasha hilo.

Baadhi ya vijana walioshiriki tamasha hilo ambalo lilihudhuriwa na vikundi 41 vya vijan a kutoka Da res Salaam, Zanzibar na Pwani, wa lisikika wakilaumu mabadiliko ya mgeni rasmi.
Chanzo: Majira

No comments: