Umoja wa Afrika (UA) (kiingereza:
African Union (AU); kifaransa: Union africaine (UA); Kihispania: Unión Africana
(UA) ; Kireno: União Africana (UA) ) ni muungano wa nchi 54 za Afrika
ulioanzishwa Julai 2002. Umoja huu unaendeleza kazi za Umoja wa Muungano wa
Afrika (kwa kiingereza: Organisation of African Union - OAU).
Nia ya umoja huu
ni kujenga muundo na mfumo wa kisiasa, kiuchumi, na kijamii ili kufikia wakati
ambapo bara la Afrika litakuwa na bunge moja, benki moja, jeshi moja, rais
mmoja, sarafu moja, n.k. Dhumuni kubwa la umoja huu ni kuungannisha nguvu za
mataifa ya Afrika ili kuweza kutatua matatizo yanayokabili bara hili kama vile
vita, njaa, ukimwi, n.k. Nchi zote za Afrika ndizo wanachama isipokuwa Moroko.
AU ilianzishwa 1963 ikijulikana kama OAU hadi sasa ni miaka 50 tangu kuundwa na
hivi leo viongozi mbalimbali wa Africa
wamesherehekea sikukuu ya miaka 50 tangu kuzaliwa. Swali ni kwamba je
wamefanikiwa kufikia malengo ya AU?
Nchi wanachama
Umoja wa Afrika ina nchi wanachama
53. Ndizo nchi karibu zote za bara la Afrika isipokuwa Moroko iliyoondoka mwaka
1985 kwa sababu ya UA ilitambua Sahara ya
Magharibi kuwa nchi ya kujitegema wakati Moroko inadai ya kwamba ni eneo la
majimbo yake ya kusini.
Mkutano wa kwanza wa Bunge la Umoja
wa Afrika ulifanyika mwaka 2004 huko Afrika Kusini.
Mikutano mikuu ya UA
Durban
(Afrika Kusini): 9-11 Jul. 2002.
Maputo
(Msumbiji): 10-11 Jul. 2003.
Sirte (Libya),
mkutano wa dharura: Feb. 2004.
Addis Ababa (Ethiopia): 6-8 Jul. 2004.
Abuja (Nigeria): 24-31 Jan. 2005.
Sirte (Libya):
28 Jun. - 5 Jul. 2005.
Khartoum (Sudan): 16-24 Jan. 2006.
Viongozi
Mwenyekiti wa UA hivi sasa Denis
Sassou-Nguesso na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya UA ni Alpha Oumar Konaré. Spika
wa Bunge la Umoja wa Afrika ni Getrude Mongella.
CHIWAMBO AUSI R,
BA SOCIOLOGY AND SOCIAL WORK,
TEOFILO KISANJI UNIVERSITY.
http://chiwambo.blogspot.com
ausichiwambor@hotmail.com
No comments:
Post a Comment