Mwanzo wa Kilwa umekadiriwa ulikuwa
mnamo 800 BK. Kuna kumbukumbu ya kimdomo inayosema: Watu wa kwanza waliojenga
Kilwa Kisiwani ndio Watakata, halafu watu wa Jasi wa kabila la Waranga. Badaaye
akaja Mrimba na watu wake. Halafu akaja Sultan Ali bin Selimani Mshirazi yaani
Mwajemi. Akaja na jahazi zake akaleta bidhaa na watoto wake. Mtoto mmoja
aliitwa Fatima binti Sultan Ali. Hatujui
majina ya watoto wengine. Walikuja na Musa bin Amrani Albedu. (kutoka BBC: The
Story of Africa - The Swahili).
Kuanzia karne ya 11 Kilwa ilikuwa
kituo muhimu ya biashara. Kuanzia karne ya 13 na 14 BK Kilwa ikawa muhimu zaidi
kuliko Mombasa.
Biashara yake ilikuwa dhahabu kutoka Dola la Mwene Mtapa (Zimbabwe),
pembe za ndovu, chuma, nazi pamoja na kununua bidhaa kutoka Bara Hindi na
Uchina. Sarafu ya dhahabu kutoka Kilwa imepatikana huko Zimbabwe Kuu.
Katika karne ya 14 -kati ya 1330 na
1340 BK- mji ulitembelewa na msafiri Mwarabu Ibn Battuta aliyeacha taarifa ya
kwanza ya kimaandishi kuhusu mji. ajengo makubwa yalijengwa ikiwa magofu yao yamesimama hadi leo kama
vile msikiti kuu, nyumba ya kifalme ya Husuni Kubwa na mengi mengine.
Kuja kwa Wareno katika Karne ya 16
ilivuruga biashara ya Waswahili. Kilwa ikarudi nyuma. Katika karne za 18. na
19. ikapata upya nguvu ya kiuchumi kutokana na biashara ya watumwa. Mwisho wa
biashara hii ulimaliza utajiri wa Kilwa.
Sehemu ya jengo ambalo lilikuwa na ukumbi mkubwa wa kunadi bidhaa zikiwemo watumwa,pembe za ndovu,simbi,mbao na vyombo vya kufinyangwa kutoka bara la Arabu na Ghuba ya uajemi,kisha kuingiza kwenye ngarawa tayari kwa kusafirisha (Maelezo haya ni kwa ajili ya picha ya hapo juu).
Kilwa Kisiwani ni jina la kijiji
kikubwa kwenye Kisiwa cha Kilwa karibu na mji wa Kilwa Masoko katika Mkoa wa Lindi, Tanzania.
Ndipo mahali pa mji wa Kilwa ya kihistoria iliyokuwa mji mkubwa kabisa kati ya
miji ya Waswahili katika pwani la Afrika ya Mashariki wakati wa karne za 12-15
BK. Kwa hivyo, Kilwa ilikuwa mji mkuu Afrika mashariki kabla ya wazungu
hawajafika kwenye bahari kuu la Hindi.
Kwa mujibu wa tariki ya Kilwa ambayo
ni miongoni mwa matini ya kizamani sana
yanayotoa historia fupi kuhusu sehemu hii ya Tanzania,
Kilwa ni mji ulioanzishwa na kusimamishwa na wahamiaji kutoka Shiraz, huko Uajemi kwa siku za leo. Ni
dhahiri kwamba matini haya ambayo jina la mtunzi wake limepotea ni aina ya
masimulizi ya kusisimua akili ya msomaji kwa kuwa na hadithi ya kibuni.
Kwa hivyo, ingawa yana maudhui ya
kuvutia sana kutokana na ushuhudio wake muhimu sana, tariki hizi hazisomeki kama
insha ya kisayansi ambayo itakuwa imeandikwa kufuatana na nadharia tete yenye
uthabiti. Mintarafu asili ya wahamiaji wa kwanza ambao walifika Kilwa, hatuna
uhakika kwamba walikuwa wanatoka Uajemi, kama
inavyodaiwa na tariki hii. Hapo tuwe makini sana.
Kwa mujibu ya tariki hizi, inasemekana kwamba
Sultani mmoja aliyeitwa Hassan bin Ali kutoka Shirazi ndiye aliyehama kule kwao
wakati wa kuibuka aina ya mgogoro kati ya watu wake. Sultani huyo akaamua
kuondoka na watoto wake sita. Kuondoka kwao huko kwenye bandari ya Siraf,
walisafiri kwa jahazi saba kuelekea Afrika mashariki. Hapo inaaminika kuwa kila
wakipita kwenye bandari ya kanda ya pwani, mmojawapo alivunja safari yake huku
akiaamua kuweka misingi ya mji wake.
Ndiyo asili ya miji saba ambayo
tunayo mpaka leo kwenye kanda ya pwani ya afrika mashariki : Mandakha, Shaughu,
Yanba, Mombasa, Pemba,
Kilwa na Hanzuân. Sultani mwenyewe alikuwa wa mwisho katika kusalia katika
msafara huu, naye akakaa kisiwa cha Hanzuani ambacho kipo Ungazija. Mikasa hii
na tukio hilo
limejitokeza katika miaka kuanzia 957 mpaka 985 baada ya K. Inaaminika kwamba
Kilwa wakati ule kilikuwa kisiwa kilichomilikiwa na wenyeji waitwao wamuli.
Kwa kuwa walikuwa hawana nguvu
nyingi, walikubali kukiuza kisiwa chao kwa kukubali kupewa vipande vya ntandio.
Hapo ndipo Ali bin Hussein alipochukua kisiwa hiki kwa ajili ya kukaa ikiwa ni
pamoja na kujenga majumba ya kujitetea dhidi ya watu wa bara na miji mingine ya
pwani.
Kati ya mwaka 957 hadi 1131, Kilwa uliwahi
kupambana na mji jirani uliokuwa unaitwa, kwa enzi zile, Shagh. Ghasia zile
zikakolea, zikawa zikageukia zikawa vita kwa ajili ya kutawala himaya kubwa.
Kilwa ukawa na sifa za fahari katika pande zote za Afrika mashariki kutokana na
nguvu zake na mali
yake ambayo ilikuwa inatoka bara la Afrika, pahala panapoitwa Sofala. Dhahabu
ya Sofala, ambayo ilikuwa ni baadhi ya madini iliyopatikana kwa wingi wakati
ule, ilikwenda kuchukuliwa na kuletwa Kilwa kwa njia ya kutembea kwa miguu.
Misafara hii ilikuwa changamoto kubwa sana
katika kutajirisha himaya ya Kilwa.
Hapo si kiwanja ila ni ukumbi amabo
mnada ulikuwa ukifanyika,au sherehe zao watawala hao wa kiarabu walikuwa
wakifanyia humo,kwa mbele kuna maji ni bahari ambapo kuna ngazi za
kuteremshia bidhaa kuingiza kwenye ngarawa zao.fika ukajionee ni utalii
nafuu zana wa kuona kisiwa cha kihistoria Tanzania. (Maelezo haya ni picha ya juu).
Hapo yupo mwandishi mwingine katika
lugha ya kiarabu, Al-Mutahar bin Tahir al Makdisi, ambaye vile vile anatoa ushahidi
mzuri wa kwamba nchi ya zenj – ambayo ni sehemu hii ya kanda ya pwani kwa enzi
hizo – ilichangia sana
katika usafirishaji wa dhahabu kutoka Kilwa kwenda Uarabuni kuanzia karne hii
ya 10.
Kwa kifupi, wataalamu wa historia
wamekubali kusema kwamba kilele cha Kilwa katika kujifaharisha kilianza karne
12 ikadumu hadi karne 15. Kilwa ikawa muhimu zaidi kuliko Mombasa. Biashara yake ilikuwa dhahabu kutoka
dola la Mwene Mtapa (Zimbabwe),
pembe za ndovu, chuma, nazi pamoja na kununua bidhaa kutoka bara Hindi na
Uchina. Sarafu ya dhahabu kutoka Kilwa imepatikana huko Zimbabwe Kuu.
Baharia maarufu ambaye pia alikuwa ni
mwana historia hodari sana, Ibn Battuta,
anathibitisha vilevile kwamba dhahabu ilikuwa inapatikana pia katika eneo
lililoitwa Yufi, nchini mwa Limi (nchi ya kiajabu ambayo wataalamu wengine
wanakisia ni pengine Nigeria).
Zama zile zilikuwa za kudhabiti utawala wa Kilwa ambao ulipanua mpaka Mafia, Zanzibar na Pemba.
Sultani Suleiman bin al-Hassan (1170-1189) aliwahi kukarabati majengo makubwa
ya Kilwa kisiwani. Anajulikana sana
kwa ujenzi aliouanzisha chini ya utawala wake ambao unaitwa Husuni mdogo.
Enzi hii bado ilikuwepo chini ya
nasaba (dynastie) ya Shirazi mpaka mwaka 1277, ambapo ni kipindi cha awamu
nyingine iliyojitokezea katika nasaba ya Mahdaliya ambayo ilitoka Hadramau, Yemen.
Karne 14 na mwanzoni mwa karne 15 zilikuwa nyenzi za fahari kubwa sana kwa sababu ya
kufaidi na kujiimarisha kipindi kile cha nyuma ambacho Sultani Al Hassan bin
Suleiman II (1331-1332) alipopata nafasi ya kuongeza nafasi ya kuswalisha
swalat al ijumaa ikiwa ni pamoja na kujenga kasri inayojulikana kwa jina la
Husuni Kubwa.
Hicho ni kiberenge kilitumiwa na mmoja
wa mwanaakolojia ambaye akikuwa akichimba ili aone masalia ya vyombo
vilivyo kuwa zikitumika wakati huo na washirazi kisiwani hao wakati
huo.aliyeshika kiberenge ni Bw.samweli mtembeza wattalii.
No comments:
Post a Comment