Monday, November 4, 2013

MAREKANI YASITISHA MISAADA WAASI SYRIA



Marekani imesitisha kwa muda misaada ya kijeshi kwa waasi wa jeshi huru la Syria-FSA.
Kamanda wa vikosi vya jeshi hilo katika eneo la kusini mwa Syria ambae pia ni mwakilishi wa waasi katika nchi za magharibi, Abu Ahmed al-Hurani, aliliambia shirika la habari la Ujerumani- DPA-mjini Amman.

Alisema alipewa taarifa mapema mwezi Oktoba kwamba Marekani haitawapatia tena misaada waasi wa FSA, si ya silaha na wala si misaada ya aina yoyote ile nyingine.
Kwa mujibu wa shirika la habari DW, duru za idara za upelelezi za Marekani katika mji mkuu wa Jordan, Amman, zimethibitisha taarifa hiyo.

No comments: