Sunday, November 17, 2013

BLOGU ZA TZ ZAGEUZWA VITUO VYA KURUSHA PICHA ZA UCHI NA NGONO?



MAKALA TIME NA CHIWAMBO
Ni siku nyingine tena wasomaji wangu wa safu hii ya Makala Time na Chiwambo nazungumuzia “Athari za Blogu na Magazeti ya Udaku hapa Tanzania”. Katika ulimwengu wa sasa hasa katika kipindi hiki cha mapinduzi ya vyombo vya habari kutoka mfumo wa zamani wa urushaji matangazo yaani “Analogia”  na kuingia mfumo mpya wa urushaji matangazo kwa vyombo vya habari yaani “Digital” mabadiliko hayaepukiki katika tasnia ya vyombo vya habari nchini.

Kutokana na hilo, Tanzania tumeshuhudia mapinduzi haya ya vyombo vya habari na kutamba kwa Blogu na Wavuti tofauti tofauti ambazo zilizo nyingi huondeshwa bila kuzilipia. Mapindizi haya ya vyombo vya habari yameleta mfumuko wa fikra tofauti tofauti katika uandishi wa makala na taarifa ndani ya  blogu zetu. 

Utafiti  uliofanywa na Mlipa Media Group inayomiliki Chiwambo’s Blog inaonyesha wazi kwamba zaidi ya asilimia 60% ya blogu zinazorusha habari hapa Tanzania ni blogu za Udaku zinazojihushisha na urushaji wa picha za ngono, Habari za mapenzi, pamoja na urushaji wa habari ambazo hazina ukweli. Pamefikia mahari hata wasanii wanapoandaa video zao picha hurushwa wakimaanisha kitu tofauti na uhalisia.

Malalamiko kama haya yamethibitishwa siku ya alhamisi pale msanii wa Bongo (Jina Limehifadhiwa) alipojitokeza mbele ya chombo cha habari cha Clouds FM kipindi kinachorushwa na Mirrard Ayo, kupinga madai ya Blogu hizo kwamba picha hizo zimepigwa wakiwa wanafanya mapenzi kumbe ilikuwa ni maandalizi ya video yake mpya aliyomshirikisha mchezaji wa mpira maarufu hapa Tanzania.

Athari za Blogu na Wavuti kwa wanajamii
Blogu kwa sasa zimekuwa ni kama vituo vya kurushia habari za Ngono, Video za ngono, Habari za Uchonganishi na za uzandiki. Pamefikia mahari hata zile Wavuti na Blogu zilizotegemewa hapa Tanzania kwa kurusha habari za ukweli na uhakika nazo zimegeuka na kurusha habari za udaku ikiwemo picha za nusu uchi au zinazoonyesha sehemu za siri za wanawake.

Wanaoathiriwa zaidi na picha hizi ni wanawake pamoja na wanafunzi. Pamefikia mahari mtu maarufu asimamapo na mwanamke au mwanaume anapigwa picha na kurushwa mtandaoni. Swali la kujiuliza, tunaelekea wapi wanahabari wenzangu? Haya ni madhara ya mtu kujua kusoma na kuandika na kujipachika kuwa yeye ni mwandishi wa habari. Yaani mtu akiweza kuandika barua naye hujiita ni mwanahabari. 

Matokeo yake ndio haya yanayoonekana leo. Blogu kama zingetumika ipasavyo kwa kuwahabarisha Watanzania wenzetu habari muhimu tungeweza kuendelea. Zipo habari nyingi za kurusha hapa Tanzania hasa huko vijijini. Magazeti, Wavuti na Blogu zetu zimeshindwa kuwafikia Watanzania waliopo vijijini ambao hushindia mihogo na uji au mlo mmoja kwa siku. Huduma zimekosekana, miundombinu kama barabara nazo ni aibu upu. Maisha ya Mtanzania leo ni ajabu, wanaishi kama wakimbizi ndani ya nchi yao.

Kwanini habari kama hizi zisirushwe ili serikali ione nini inachowafanyia wananchi wao. Ijapokuwa kuna Uhuru wa kutoa na kupokea habari, hatuna budi vyombo vyetu kuwa vyombo vya habari vya watanzania “The voice of the voiceless”.  Badala yake tumevigeuza vyombo hivi na kuwa vituo vya kuandika habari za ngono. 

Kama leo hii ningeulizwa swali moja tu na mtu yeyote kuhusu nini kinachokukera ningesema “Vyombo vya Habari vya Udaku hasa Blogu” na ningependekeza vifungiwe ili kulinda utu wa watu wetu. Hivi jiulize swali moja tu. Je ungependa watoto na wajukuu wako wazione picha zako za ngono? Huko  ndiko tunakoelekea kwa sasa. 

Athari za blogu hizi ni kwamba, tunawafundisha watoto wetu  kuingia katika ngono na biashara ya ngono wakiwa na umri mdogo sana. Hivi kama wewe ni mwandishi wa blogu, utajisikiaje pale utapoikuta picha ya mtoto wako imetupiwa pale ndani ya blogu yako au nyinginezo? 

Wanafunzi na picha za ngono mtandaoni
Wanafunzi wetu kuanzia sekondari hadi vyuo vikuu imekuwa ni fasheni kwa baadhi yao kupiga picha za uchi na ngono na kuwapa wanablogu au kuzivujisha mtandaoni. Wasomi wa leo na wa jana ni tofauti kabisa. Wasomi wa jana waliheshimu sana utu wao na tamaduni za kitanzania lakini wa leo hawajiheshimu baadhi yao hasa wasomi wetu wa kike. Hivi baba yako akibahatika kuiona picha yako ukiwa uchi au unafanya ngono atajisikiaje au wewe utajionaje?  Hao ndio wasomi wetu wa leo. Somo la maadili limekuwa kikwazo kwao. Tunatengeneza taifa la weusi lenye giza mbele yake. 

Nini  kifanyike kuzuia uvunjifu wa sheria
Swala kubwa ni wanablogu wenyewe kujiheshimu kwanza. Kuthamini watu wengine na kujithamini wenyewe. Wanablogu wawe wakwanza katika kupinga urushaji wa picha za ngono zinazozidi kusambaa mtandaoni siku hadi siku. Mwanablogu pekee ndiye anayeweza kuzuia blogu yake isiweke picha za ngono ili kuweza kuzuia wimbi la watoto wadogo kutembelea kwenye picha kama hizo. 

Kitu cha ajabu ni kwamba baadhi ya hao wanaorusha na kuongoza blogu hawajui sheria za kujilinda pale watapokubwa na kesi juu ya wanachokiandika yaani “Law of Defamation and its element. 

Haya yote ni madhara ya mfumo wetu wa elimu na inaonyesha namna gani watanzania hawajakombolewa na elimu. Bado tupo ugenini katika elimu. Tunafanya elimu yetu kama kitu kisicho na umuhimu. Tunapeleka wapi elimu yetu? Tunatengeneza “Taifa la Vilaza, Mambumbumbu, na Majuha” na hao ndio viongozi wetu hapo baadaye sisi tutapoaga na kuondoka.
Imeandikwa na Ausi Chiwambo

Phone No. 0753110740

Tuesday, November 12, 2013

IRAN YASISITIZA URANI ITARUTUBISHWA



Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema haki za nchi hiyo za kurutubisha madini ya urani ni mistari mekundu ambayo haiwezi kuvukwa.
Pia amesema Jamhuri hiyo ya Kiislamu ilitumia busara wakati wa mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa nchi hiyo hivi karibuni.

Akizungumza katika Bunge la taifa hilo jana, Rais huyo alisema wamewaeleza wajumbe wanaozungumza nao kuhusu mpango huo wa nyuklia kwamba hawatosalimu amri kwa vitisho vyovyote vile, vikwazo, hila au kwa kubaguliwa na kwamba nchi hiyo haikuinamisha na haitoinamisha kichwa chake kutokana na vitisho kutoka mamlaka yoyote ile.

Alisema kwamba, kuna mistari mekundu ambayo haiwezi kuvukwa na masilahi ya taifa ni mistari mekundu yenye kujumuisha haki chini ya mifumo ya sheria za kimataifa na kurutubisha urani.
Hata hivyo, juzi mataifa sita yenye nguvu duniani yalishindwa kufikia makubaliano ya kusitisha mpango wa nyuklia wa Iran.

Aidha, yalidai tofauti zao zimepunguwa na wataanza tena mazungumzo katika kipindi cha siku 10 kujaribu kuumaliza mzozo huo uliodumu kwa muongo mmoja.

CHADEMA: HATUHUSIKI MADAI YA ZITTO



Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema Ofisi ya Katibu Mkuu wa chama hicho imepokea barua iliyoandikwa na Naibu Katibu Mkuu, Bw. Zitto Kabwe.

Barua hiyo, inamtaka Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Wilbrod Slaa athibitishe madai ya ripoti inayosema“Taarifa ya Siri ya CHADEMA”iliyosambazwa katika mitandao mba limbali ya kijamii.

Taarifa hiyo inadai kuchunguza mwenendo wa Bw.Kabwe tangu mwaka 2008-2010 na kubaini amepokea fedha kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuivuruga CHADEMA.
Akizungumza na Majira jana, Ofisa Habari wa CHADEMA,Tumaini Makene,alise ma barua aliyoiandika Bw. Kabwe itafanyiwa kazi kwa mu jibu wa taratibu, kanuni za katiba ya chama.

“Chama chetu kinaongozwa na vikao hivyo barua yake itafanyiwa kazi...CHADEMA h aiendeshwi na taarifa za magazetin i au mitandaoni,”alisema Bw. Makene.
Aliongeza kuwa,si mara ya kwanza makundi yasiyojulikana kusambaza taar ifa za kutaka kumchafua Bw. Kabwe k upitia mitandao hiyo ambapo Ofisi ya Habari,ilishughulikia suala hil o na kuhakikisha taarifa hizo zinaondolewa.
“Hivi sasa ni mara ya pili, Bw. Kabwe anali fahamu hilo hivyo CHADEMA hakihusiki, lakini kitashughulikia suala hili kupitia vikao ili kupata majibu sahihi,” alisisitiza Bw.Makene.

Katika taarifa yake aliyoitoa juzi kwa vyombo vya habari, Bw.Kabwe alisema taar ifa hizo zimesambazwa katika mitandao ya kijamii hiv yo alimtaka Dkt.Slaa, athibitishe kinachoitwa“Ta arifa ya Siri ya CHADEMA”,kama ni taa rifa ya chama au kiikanushe ili kumpa fursa ya kuchukua hatua za kisheria dhidi ya waandishi wa taarifa hiyo.
Hata hivyo, Bw. Kabwe ambaye pia ni Mbunge w a Kigoma Kaskazini,aliziita taarifa hizo za kutunga zilizojaa uongo wa kiwango cha kutisha hali ambayo imemfedhehesha, kumsikitisha na kumkasirisha.

Alisema taarifa hizo ziliibuliwa katika kipindi am bacho alikuwa safarini kutetea haki za Watanza nia na Afrika ambao utajiri wao wa rasilimal i unafaidiwa na watu wachache waliohifadhi fedha katika akaunti nje ya nchi.
Chanzo: Majira

NITAMNG’OA SPIKA MAKINDA-MBUNGE




Mbunge wa Nzegamkoani Tabora ,Dkt.Hamisi Kig wangalla ,amesema bado ana dhamira ya kuwasi lisha hoja ya kumng’ oa madarakani Spika wa B unge, Bi.Anne Makinda.
Alisema uvumi ulioenea kuwa hoja yake imeondolewa kwa agizo la Chama Cha Mapinduzi (CCM), hauna ukweli.

Dkt. Kigwangalla aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika mkutano wa hadhara u lioshirikisha wakazi wa jimbo hilo na vitongoji vya ke uliofanyika katika Uwanja wa Parking.

Katika mkutano huo, Dkt. Kigwangalla aliulizwa swali na mkazi wa jimbo hilo kama kweli ana ubavu wa kumng’oa Bi.Makinda, anayetoka na na chama chake.
“Mheshimiwa mbunge,naomba utu thibitishie kama una uwezo wa kumng’oa Spika wa Bunge (Makinda), kama ulivyotangaza dhamira ya kuw asilisha hoja binafsi bungeni ili bunge liweze kumng’oa.

“Kwa jinsi tunavyofahamu utaratibu ndan i ya CCM, huna ubavu wa kufanya hivyo , ina onesha ulikuwa ukijifurahisha tu,”alihoji mwananchi huyo.
Mwananchi huyo aliongeza kuwa, kwa kawaida CCM ina utaratibu wa kuzuia hatua mbalimbali zinazotaka kuchukuliwa na wanachama wake hivyo alimshauri Dkt.Kigwangalla, aacha ne na hoja hiyo kwani hana ubavu wa kumng’oa Bi.Makinda.

Akijibu swali hilo,Dkt. Kigwangalla alisema,si kw eli kwamba CCM ina utaratibu wa kuondoa kin yemela hoja ambazo haikubaliani nazo ambapo suala la kutaka kumng’oa Bi. Makinda lipo ndani ya uwezo wake na kufafanua kuwa, ho ja hiyo haijaondolewa na hivi sasa ipo katika hatua za mwisho ili iweze kufikishwa bungeni.

“Kwa hili la kumng’oa Spika wa Bunge,niwaele ze wazi kuwa si kweli linaweza kunishinda... hoja imewasilishwa na Bi. Makin da atang’oka kama nikiamua kuendelea nayo kwa sababu tayari hoja nimeiwasilisha na nimekidhi masharti yote.
“Hivi tunavyoongea, hoja yangu tayari imeto ka hatua ya kwanza na kukidhi vigezo vyote sasa inaenda hatua ya pili ambayo Kamati ya Bunge y a Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge,itaamua hoja yangu iingizwe bungeni au isiingizwe,”alisema .

Aliongeza kuwa,baada ya hapo utafuata mcha kato wa mwisho ambao ni hoja hiyo kufikishwa bungeni na yeye kuiwasilisha rasmi mbele y a Bunge ili kufanyiwa uamuzi na wabunge wote kwa kupiga kura na kama atashinda au kushind wa,hilo ni jambo lingine.
Dkt.Kigwangalla alisema uamuzi wa kuo ndoka au kutoondoka kwa Spika, kutategeme au amuzi wa wabunge wenzake na kusisitiza kuwa , CCM haiwezi kuzuia hoja hiyo bila ya kupatiwa uamuzi na wabunge wote.

Akijibu swali ambalo lilihusiana na fedha za ushuru wa huduma zilizotolewa na Mgodi wa Dhahabu wa Resolute, ulioko wilayani humo, Dkt. Kigwangalla alisema fedha hizo sh.bilioni2.340,zililipwa na mgodi huo na s asa zimehifadhiwa katika akaunti maalumu ili baadaye zitumike kama mtaji wa kuanzishia Benki ya Maendeleo ya Wananchi wa Nzega.

“Fedha hizi tulizipigania kwa kiasi kikubwa hadi kuandamana lakini tulifanikiwa kuzipata, niwathibitishie zipo salama katika akaunti maalumu tuliyoianzisha ili baadaye ziweze kuanzisha Benki yetu ya Maendeleo ambayo itaweza kutupa mikopo ya kuendesha shughuli zetu,”alisema .

Alisema lengo lake ni kuhakikisha fedha hizo zinatumika vizuri ili kuwasaidia wananchi w a Nzega kubadilisha maisha yao ambapo watu watahamasishwa kujiunga katika ushirika au SACCOS ili waweze kupewa mikopo p ia zitatumika kununulia mitambo ya kutengeneza barabara na uchimbaji visima vya maji.

Gazeti moja linalotoka kila siku (si Majira), liliandika habari inayosema Dkt. Kigwangalla anadai Bi. Makinda amekiuka kanuni kwa kuidhinisha malipo ya sh. 430,000 kama posho kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, tofauti na wajumbe wa kamati nyingine ambao malipo yao ni sh. 180,000 kwa siku.

Hoja hiyo ilipingwa vikali na baadhi ya wabunge akiwemo Mbunge wa Tabora Mjini, Bw. Ismail Aden Rage (CCM) na Mbunge wa Kigoma Kusini, Bw. David Kafulila (NCCR-Mageuzi) ambao walidai hawaoni sababu ya kumuondoa Bi. Makinda madarakani.

Bw. Kafulila alisema hilo ni suala la wana-CCM, kwani Bi. Makinda aking’olewa madarakani, mtu ambaye ataziba pengo lake hawezi kutoka upinzani. Hoja hiyo ya Dkt. Kigwangalla iliibua mjadala kwa baadhi ya wabunge na wengine kukataa kusaini karatasi ambayo walipelekewa ili kuunga mkono.

Mbunge wa Ludewa, mkoani Njombe, Bw. Deo Filikunjombe, alisema hoja ya Dkt. Kigwangalla imejengwa katika msingi hafifu isiyozingatia masilahi mapana ya nchi na mtazamo finyu.
Chanzo: Majira