Friday, August 9, 2013

PICHA ZA BANDA LA HALMASHAURI YA WILAYA YA TUNDURU KATIKA MAONYESHO YA NANE NANE HAPA MKOANI MBEYA. PALIVUTIA SANA

Hili ndilo jengo la Halmashauri ya Wilaya ya tunduru hapa mkoani Mbeya ndani ya majengo ya Nane nane.
 Wanatunduru pia Waliweza kutengeneza Ghala la kihifadhia mahindi, Nyugu, Karanga na Vnginevyo kama   unavyoliona kwa kiruga tunaita "CHIKUTI" katika picha tatu kushuka chini



 Hapa Chini ni picha ya friji ya Asili iliyoandaliwa na Wenyeji wa Wilaya ya Tunduru huko Mkoani Ruvuma katika maonesho ya Nane nane. Humu Ndani unaweza kuhifadhi Maji, Soda, Juice, Nyama na Vile vingine unavyoone vinafaa kuwekwa kwenye friji. Friji hii imetengenezwa na Mkaa wa miti

 Hii ni Bustani mfuko Ambapo mfuko huwekwa Samadi na Mchanga na kupandikiza mboga mboga.


                                                              Bustani ndani ya Tenga
                                   Mwonekano Halisi wa ustani ya Mfuko baada ya kupandwa vitunguu.



 Hii ni Bustani mlima kama inavyoonekana Hapo. Hicho ni kichuguu au mlima uliotengenezwa na kupanda chochote kile upendacho. Amakweli Palivutia

 Hapa chini ni Majengo ya Kufugia ng'ombe kama yanavyojieleza. Anayeonekana ni Rafiki yangu Bwana Sunh Emmanuel akiangalia technologia ya Tunduru









                                    Hapa chini ni Mabanda ya kufugia kuku yaliyojengwa kisasa






 Wananchi Mbalimbali Wakipata somo namna ya utengenezaji mbolea ya Asili inayozalishwa Tunduru yetu
                               Huu ni mfano wa tanuli lililotengenezwa kupata mbolea ya Asili
ELIMU HII UNAWEZA KUIPATA KUPITIA NAMBA YA BLOGU HII YA MATANGAZO

No comments: