Saturday, December 22, 2012

HOTUBA YA MBUNGE WA BASO MH. TWEVE NEHEMIA J.

HOTUBA NILIYOITOA TAREHE 21 DECEMBER 2012 JIMBONI KWANGU;
Waheshimiwa, viongozi wa darasa Bugoya Ally I, na makamu wako Sara Samwel.
Waheshimiwa, viongozi wa TEKUBA, mabibi na mabwana.
Awali ya yote napenda kumshukuru mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na mwenye kudra juu ya maisha mema.
Pole zangu ziwafikie wenzetu woote waliofikwa na matatizo katika kipindi choote cha nyuma hadi tulipo sasa.
Baada ya yote napenda kutoa shukrani zangu za dhati sana kwenu nyote kwa kutosimamisha mgombea mwingine yeyote katika nafasi ya ubunge wa jimbo letu, Hii ni kuonyesha imani mliyonayo juu yangu na nafasi ya uwajibikaji wangu ndani ya serikali ya wanafunzi ya chou chetu, Ni uhakika wangu kuwa hamkufanya kosa kwani nimehakikisha ninawatumikia wananchi wangu kwa kadri ya uwezo wangu na mamlaka yanguu ndani ya ofisi ya bunge na pia hata katika ofisi ya wizara ya mikopo.
Ndugu zangu nilipoteuliwa kushika nafasi ya kuwa naibu waziri wa pili wa mikopo nilijisikia vizuri kwa sababu ni nafasi adhimu si kwa Tweve bali kwa kitengo chetu cha elimu jamii, kwa maana hiyo basi sisi kama watu wa elimu jamii tunayo adhima kubwa ya kuwatumikia wananchi kwani vyeo tulivyonavyo ni dhamana.
Salamu zangu za pongezi ziwaendee pia BUGOYA ALLY I na SARA kwa kuchaguliwa kuwa viongozi wapya wa darasa letu, kwani hadi sasa uongozi wao umefana na mimi kama mbunge ninatoa kauli yangu kuwa hakuna kiongozi anayeweza kuonekana mzuri kwa watu wote pindi anaposhika hatamu (uongozi)
Napenda kutumia fursa hii kipekee sana kumshukuru Mh. Chiwambo na makamu wake Mote Dorothea ambao ni wastaafu kwa sasa, utumishi wao ni mzuri na tena umetukuka, hongereni sana.
Ndugu zanguni, wanafunzi wenzangu, ilihali hatuwezi kukaa na makaa ya moto yakiwa mifukoni mwetu ni lazima tufikie hatua ya kujadili baadhi ya mambo mahususi ndani ya letu, ni wiki chache tu nilipotoa namba yangu ili watu waweze kutuma mambo mbali mbali yanayohusu jimbo letu.
Ifahamike kwamba ni matarajio yangu makubwa kuwa hotuba yangu haitokuwa kichochezi cha kuwamega wanabaso wala kuwatenga kutoka kwenye umoja uliopo hivi sasa, Bali hotuba hii fupi inalenga kuweka msingi wa umoja endelevu, ushirikano upendo na mshikamano;
Ndugu zangu nilitoa fursa hii ya kunitumia mambo mbali mbali kupitia njia ya simu kwani mtiririko wa maswali ambayo pengine sikuwa na majibu yamezidi na huku mambo niliyonayo ni mengi sana kwa hiyo nilishindwa kuyajibu na kuamua mkutano wa pamoja ambao tunaufanya leo. MAMBO HAYA NI:-
v Mchango wa TEKUBA ni mkubwa kiasi cha kuathiri utayari wa watu kuchangia kwa uhakika, na hata katika michango hiyo inaonekana dhahiri kuwa madhumuni yamejikita katika starehe na sio katika kusaidiana sisi kwa sisi na hata hivyo ni jukumu letu sote kushiriki katika utoaji wa maoni ya katiba ya TEKUBA.
v Michango inayohusu kufiwa ipewe kipaubele hasa kwa pale matatizo ya kufiwa yanapokuwa ni very sensitive kwa muhusika wa tukio la kufiwa, na ikumbukwe kuwa wananchi wanataka ufuatiliaji wa michango ufanyike chini ya uongozi unaotambulika na unafahamika kwa wote na hata hivyo michango ya pongezi kama vile kwa mtu aliyejifungua, na kutuma pongezi za aina yoyote ile ifanyike chini ya uhiari wa mtu na si kufanya ulazima na kutangaziana matangazo kwa kuhimiza ulazima wake.
v Na kwa wale wenye mashine/computer wafanyike msaada kwa wenzao na sio kufanya mashine kuwa chanzo cha mapato ilihali hawafanyi biashara yoyote mfano mzuri ni pale mtu anapoamua kuwatoza wenzake hela kubwa kwa kiasi cha zaidi ya Tshs 5000 na katika hali ya kawaida hakuna kazi inayoweza kuchapwa kwa hela hiyo na hili linaambatana na suala la kukataa kumwandika mtu jina ilihali yupo tayari kuchangia hela ya kuprint kazi na kueleza kile kilichomfanya asiwepo katika mchakato wa kufanya kazi hiyo.
 Mwisho kabisa kwa mapenzi ya dhati kabisa napenda kusisitiza kitu kwenu wenzangu kuhakisha kwamba tunakuwa watu wa mbele kutembelea blog yetu ambayo mmiliki wake yundani yetu, mimi kama mbunge ninachukulia kama ni blog yetu sote na ninajivunia sana kwani ni kitu cha msingi kufanywa na mwenzetu mpendwa na ninaona ni mtu kwanza pengine kufanya kitu kama hiki ndani ya kitenngo cha elimu jamii.
Aidha mimi kama mbunge napenda kuwahimizeni nyoote kujiunga na Asasi ya umoja wa mataifa iliyo na tawi lake hapa chuoni kwani ni muhimu kwetu kama watu wa elimu jamii.
NAWATAKIA SAFARI NJEMA NA SIKUKUU NJEMA ZENYE BARAKA TELE, MUNGU IBARIKI BASO, MUNGU IBARIKI TEKU, MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRICA.
NINAOMBA KUWASILISHA.
 
TWEVE NEHEMIA J (MBUNGE NA NAIBU WAZIRI WA MIKOPO)
P O BOX 20,
NJOMBE, TANZANIA.
ntweve@gmail.com
 +255776047873

Thursday, June 21, 2012

BUSARA ITUMIKE KUZUNGUMZIA MGOGORO WA ZANZIBAR

BUSARA ITUMIKE KUZUNGUMZIA MGOGORO WA ZANZIBAR
Chiwambo Asi R.
Zanzibar mwishoni mwa wiki iliyopita tulishuhudia machafuko makubwa sana. Ikihusisha vitendo vya uchomaji wa makanisa, uhalibifu wa mali za umma, na wengine kuwekwa ndani. Hili si jambo tu la kukurupuka na kuanza kubeza sana upande mmoja kwani kila jambo ni matokeo ya mfumo Fulani.

Taasisi iliyoingia kashfa hiyo ni Taasisi ya UAMSHO ikiwa chini ya baadhi ya waislamu Zanzibar. Zanzibar wanataka nchi yao iwe huru, wakati watanganyika tunataka Zanzibar iendelee kuwa hru. Na cha kusikitisha zaidi lile baraza la usuruhisho masuala ya muungano ni raia wa Zanzibar. Hakuna Mtanganyika pale.

Ofisi inayohusika na masuala ya muungano ni ofisi ya Makamu wa rais. Na hata walio kwenye kamati hiyo wote ni  Wazanzibar. Hivi unadhani kama ikitokea wao hawautaki muungano unadhani kwamba wataleta majibu yaliyo sahihi? Hawa ni viongozi wetu, tuendelee kuwaamini kwani tushike ule usemi usemao kiongozi ni kioo cha jamii.

Makundi yeyote yanavyoanzishwa huanza na  Hatua (stage) zake. Kila hatua inajitegemea kama ifuatavyo:-
  1. Hatua ya kwanza ya kuunda Kikundi. (Preliminary or incipiency stage). Hapa ndipo vichwa vya watu vinapogongana kimawazo juu ya kit Fulani kwenda tofauti. Viongozi hutokea ambao si rasimi na kuanza kuonesha hisia zao.
  2. hatua ya pili ambayo inahsisha kuanza kutengeneza kundi na kuongeza uelewa kwa watu (Coalescence stage). Hapa panahitaji viongozi ambao wataongeza ukaribu na watu wengine. Kipindi kingine wanazungumzia mawazo yao yote hata kupitia vyombo vya habari.
  3. hatua ya nne ambapo kikundi kimekomaa na kufikia kilele cha kundi (Institutionalization or Bureaucratization stage). Hapa viongozi wanakuwa ni wakuchaguliwa na ufata mfumo wa taasisi Fulani (chain of command). Na viongozi hao hulipwa kiasi cha fedha.
  4. Anguko. (Decline stage).hapa ni sehemu ya mwisho kabisa ambapo ni anguko ku la kundi lililoundwa katika hatua ya kwanza. Hapa kundi hili usambaratika kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kufanikiwa kwa lengo lao, au kusambaratishwa.

Hizo ndizo hatua za makundi yanavyotokea. Hivi viongozi wetu hawakuziona hatua kama hizi? Kama kweli tunautaka muungano kwanini serikali iliwaachia uhamsho kuendesha mijadala yake huku wakijua kuwa wanazidi kulikuza zaidi kundi hili? Huu ni uasi au ni nini? Kwa upande wangu naona kwamba ni uzembe wa watu wachache ndio uliopelekea visiwa vya Zanzibar kuingia kwenye machafuko.

Kwa kiongozi yeyote aliyesomea masuala ya uongozi au jamiii lazima amezisoma hatua kama hizi na namna ya kuyasambaratisha haya makundi. Kwanini zisitumike ikiwemo njia za amani. Makundi haya yalipata uchungu zaidi pale viongozi wa taasisi zisizo za kiserikali walipokamatwa na jeshi la polisi katika eneo la bunge kwa madai kuwa ni kinyume na sheria za nchi kwa kifupi nilivyoelewa mimi ni kwamba walikuwa waasi. Ni kweli kabisa.

Lakini ilipaswa itumike busara kutatua mgogoro huu badala ya vitisho. Hawa Wazanzibar walianza kudai Zanzibar ijitenge kwa muda wa miaka mingi sana. Kwa wale wenye kumbukumbu munaweza kumkumbuka yle aliyekuwa rais wa Zanzibar Ndugu Aboud Jumbe Mwinyi alivyotangaza nia ya kutaka kuvunja muungano akiwa Dodoma kwenye vikao Fulani. Kilichompata ni kuondolewa klatika nafasi hiyo.

Nyadhifa zake zote za kichama na serikali alivuliwa kufumba na kufumbua macho. Hii ni kweli kuwa uasi ulianzia muda mrefu sana. Hapo ndipo Mwalimu Nyerere aliposema kuwa tusikubali kuvunja muungano. Hata Nyerere wetu kumbe aliyajua haya mapema hasa pale kundi la G51 lilivyoanza kukua nchini Tanzania.

Kwa hiyo suala la hawa jamaa wa UAMSHO chanzo chake kimetoka mbali. Kwa hiyo kwa wakati huu ambao nchi mbalimbali zinaonyesha namna waasi wanavyoongezeka siku hadi siku, hasa nchi zile za kiarabu na baadhi ya nchi za Kiafrika, napendekeza serikali bora itumie busara zaidi katika kutatua tatizo hili badala ya vitisho na nguvu nyingi. Kweli hawa watu wapo kinyume cha sheria za nchi.

Lakini busara muhimu zaidi kuliko nguvu zaidi. Kwanini serikali isikae nao pamoja na kanza kusikiliza madai yao? Kama yana msingi kwa hatima ya nchi yetu yafanyiwe kazi. Mbona madaktari ilitumika njia kama hii. Kwanini isitumike kule Zanzibar. Inasikitisha kuona kila kukicha vituko Zanzibar mara tunataka nchi yetu.

Haya yamefugwa sana na sisi wenyewe kwani viguvugu lilipoanza hasa katika ule muswada wa maoni ya katiba mpya hawa walichana hadharani na kupinga kujadiliwa. Wakati ule likuwa muhimu kuweza kutafta njia mbadala za kutatua ili kuonyesha namna tunavyoujali muungano wetu.

Nalipenda sana Tanzania hasa hili jina zuri la Tanzania. Kwa hiyo nadhani viongozi wa serikali mutatumia wawazo haya ili kuhakikisha tunabaki na Tanzania moja, Imara na yenye amani na utulivu kama aliotuachia mwalimu Nyerere.

Powered by Chiwambo Ausi R.       

MWANAHARAKATI NA TANZANIA YA LEO

MWANAHARAKATI NA TANZANIA YA LEO

Hapo mwanzo katika kijiji kimoja kulikuwa na vijana wenye nguvu na waliopigania nchi yao kuwa huru. Nchi hiyo ilijulikana kwa jina la Kuabudika, na ilikuwa na miji mikubwa kama sita. hali ya jiji la kwanza ilikuwa sawa na yale mengine. kila kukicha nchi hii maarufu kwa utajili wa kila aina ilibadilika. maisha yalikuwa bora ya jana kuliko leo kikicha. nimesahau kuanza na neno hili "hadithi hadithi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!" hadithi hadithi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!".

yale majoho waliyozoea kuvaa kila siku wale wenye nazo ilifikia mahali bei ilipanda kiasi kwamba kama ni mfanyabiashara ndogondogo ununuapo joo moja fedha za mtajiulikuwa kwaheli. watu walilalamikia juu ya nchi yao. Nchi hii ilikuwa na sifa kubwa yenye viongozi wanaotabili nini hapo baadaye kitatokea na nani aondolewe wapi hapelekwe wapi. kiongozi aliyeamishwa akikataa kufanya hivyo hatima yake ilikuwa ni kifo tu.

Hali ilikuwa vile hadi walipozaliwa watoto mapacha watatu waliofanana kwa kila sifa. walikuwa wakakamavu, wazuri, wenye nia ya kukomboa nchi yao na walitembea wakati wote pamoja. walitumia muda wao wote kusoma kuanzia darasa la kwanza hadi la nane wakiwa na wazazi wao wateule. watoto hawa walipendana sana, walivaa sare vizuri ijapokuwa uwezo wao ulikuwa mmmmmmmmmmm.

Mungu aliwabaliki wale watoto watatu na kufahuru darasa la nane shule ya msingi Majaribu iliyoko wilaya ya Chinyauleje kata ya Kweko. walichaguliwa kuingia kidato cha kwanza na kumaliza kidato cha nne shule ya sekondari Achimwene. mungu aliwabaliki kusomea masomo ya uasikari katika kikosi maalumu. majina ya wale wote yalikuwa "HUZUNI, AMANI NA UTULIVU". baadaye walifanikiwa kwenda kikosi kingine cha masomo ya juu ya uasikari na kuwa makomando wa jeshi.

Hawakulidhika na mishahara waliyopewa kwani walikuwa na ndoto ya kuikomboa nchi yako. Vijana hawa waliamua kuacha kazi na kuendelea na masomo ya chuo kikuu. walisoma chuo kikuu cha Mwanaharakati kilichopo nchi nyingine ya Ahadi. walisoma masomo ya "BA-political science and International Relatioship".

baada ya kutunukiwa Shahada zao walirudi Nyumbani Nchi ya "Kuabudika". siku ile ilikuwa siku ya ajabu kubwa sana. vijana walifuatwa na ndege ya Wanamapinduzi. safari ilianza saa sita mchana. safari ile ilikuwa ni ya siku mbili. waliingia nchini mwao mnamo saa 8.00 mchana. nchi ilianza kutikisika ghafla kabla ndege kutua uwanja maarufu wa St. Ambuje. Mchana kukawa giza nene kama manane ya usiku. nchi ilikuwa nyeusi ikiashiria kuingia kwa wakombozi watatu kutoka Mwanaharakati university.

Ndege ilitua chini, ghafla mchana ulilejea. Kiongozi wa nchi lle maarufu kwa jina la NJETE JA KWEKULA", ALIAGIZA VIJANA WALE WATATU WAUWAWE HARAKA IWEZEKANAVYO KWANI MTABRI WAKE MAARUFU ALITABIRI KUWA VIJANA WALE WA WATATU MMOJA KATI YAO ATAKUWA MTAWALA WA NCHI LE.

ikumbukwe kuwa yule raisi alijiweka madarakani ni kiongozi wa maisha. hakukuwa na uchaguzi wa rais katika nchi ile, yeye aliteua wabunge na viongozi wote wa serikali. yeye ndiye Hakimu na jaji mkuu wa nchi ile. na wazizi wa wae watoto waliuawa na rais wakati watoto hawa wakiwa wachanga sana baada ya rais wa nchi hiyo kuwatuhumu kwa kutaka kufanya mapinduzi.

Wakiwa uwanja wa ndege wale vijana watatu waliwekwa chini ya ulinzi na kikosi maalumu cha makomandoo. ilikuwa patashika vijana wale kukamatwa. vurugu kali ilitokea. na wakati huo huo watu walikuwa wamejaa barabara zote kuzunguka kiwanja maarufu cha ndege. barabara zote zilijaa watu kwa kuwa waliona wanamapinduzi walikuwa wanaingia siku ile. vijana wale walitakiwa kuzungumza na wananchi ili kuzungumzia nini hatima ya nchi yao ambayo uchumi ulishuka kiasi kwamba thamani ya fedha ilishuka hata mkate ulikuwa haushikiki kwa bei mbaya.

wote watatu walikamatwa palepale uwanja wa ndege na kupandishwa ndege maalumu ya jeshi na ndege kupaa tena kuelekea uwanja wa dhambi tayari kwa kunyongwa kama hukumu inavyonesha.

wakati ule vyombo vya habari vilikata matangazo ghafla. wananchi walishangaa sana kuona mgeni wao anapandishwa ndege ya kijheshi na kupaa juu. ghafla mabomu ya machozi yalianza kuvuma huku na kule. watu waliuwa sana. yale yalikuwa mauaji makubwa kuliko yote Tangu nchi ile Iumbwe na Mwenyezi Mungu.

watu waliuwawa makanisani, misikitini, mitaani na maeneo yenye mkusanyiko. hali ilikuwa mbaya tena mbaya sana. watu milioni moja waliuwawa. hapo ndipo sheria mbaya zaidi zilivyoongezeka. katiba ya nchi ilibadilishwa na kunyima uhuru wa vyombo vya habari, maandamano pamoja na mikusanyiko.

siku ile ya mauaji umji ulijaa maiti kiasi kwamba watu walisema leo ndio mwisho wa dunia. Miezi ishirini na nne ilipita, hatima ya nchi haijulikani. wannchi hawajui wale wakombozi wao wamepelekwa wapi. na mtu hana haki ya kuongea juu ya mstakabali wa nchi yao. watu waliamini mungu ndiye aliyesababisha hali hiyo ya nchi. nchi ilikuwa maskini ya mwisho katika dunia ile. watu waliishi bora jana kuliko leo na walikuwa wanasubiri kufa tu maana hakukuwa na namna ya kuwezakuendesha nchi yao.

vijana wale baada ya ya safari ya siku mbili wafikishwa msitu mnene wa "CHIKANJE". msitu ule watu huwa ni chakula cha wanyama. wale askari waliopewa kazi ya kuwanyonga wale vijana watatu, walianza kuwaambia kuwa "nyinyi mlikuwa ni makomandoo wa jeshi, mliacha kazi ya uasikali kwenda masomoni ili kuikomboa nchi yetu. na rais wa nchi hii ametoa amri ya kuuawa kwenu. mnatakiwa muuawe mara moja................................................................................................................. ni amri.

mungu si athumani. mungu amtupi mja wake. wale asikari wanyongaji walikaa kikao cha ghafla. loo!!!!!!!!!!!!. askari mmoja alisema "haiwezekani watu hawa wauawe". mmmmmmmmmm! la hasha!!!!! penye nia pana njia. askari walitafakari na kufikia hatima ya wale vijana watatu. askari wale waliamua kuwaachia huru wale vijana watatu kwa masharti maalumu.

Walikaa kikao cha ghafla na wale watuumiwa watatu. waliwafungua pingu na kuanza kupanga mikakati ya kuipindua nchi. waliweka kila njia na mipangoyote ilikaa vizuri. walipanga wale watakuwa na ulinzi wa jeshi la nchi hiyo. katika mikakati yao ilikuwa ni kumteka kiongozi wa jeshi wa nchi ile na kisha kumalizia kwa rahisi. haraka haraka haina baraka, mmoja wa askari kwa cheo cha Copro Antinion Mwangatu-mbujiko. kazi ilianza mara moja.

kama mungu alipanga hivi. wananchi wa nchi ile waliamka asubuhi bila ya kuamshwa na kuanza kuandamana bila ya kiongozi. kila kijiji, katani, wilaya ,miji na majiji yaliandamana. watu walikuwa wachungu kama pilipili kichaa. Habari ndiyo hiyo kila kona ya jiji. Wananchi walibeba mabango yaliyoandikwa "MAPINDUZI NI LAZIMA, RAIS HATUKUTAKI, LAZIMA UONDOKE, PIGA UA GALAGAZA NCHI HII SI YAKO, RAIS ONDOKA TUPATE AJIRA NA  mengine mengi". kumbe hali ile ilitengenezwa na jeshi la nchi ile na wale vijana watatu wa chuo kikuu.

Askari wote wa nchi waliwatetea wananchi, hakuna aliyeuawa na askari kama ilivyokuwa mwanzo, katiba haikufuatwa kwa askari kuruhusu wananchi waandamane, na kuwapa mabango. kipindi wananchi wakiandamana jeshi la nchi hiyo ilimteka kamanda wa jeshi la nchi hiyo Meja General MWE ULI.

Rais alishangaa ghafla kuona wananchi wanakaribia kasili wakiwa na mabango ya ya maandamano pamoja na silaha kali wakisindikizwa na jeshi la nchi hiyo huku ndege za jeshi za kiita zisizo na rubani na zenye rubani zikiwa na siraha nzito nzito ikiwemo mabomu mazito mazito.

wananchi wa nchi ile walifanikiwa kuiteka ikuru na kumchoma moto Rais wa nchi ile. habari yake iliishia pale. mara ya mwisho yule rais kabla ya kifo chake alisema "KWELI NGUVU YA UMMA..................................................................................................................................................................."

LEO HII NAUKUMIWA BILA KUTAKA KISA UONGOZI WANGU ULIKUWA MBAYA" MUNGU NISAIDIE NIFIKA PAHALA PEMA PEPONI" Wananchi walisema "ameeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee" wengine walisema Amina". 

POWERED BY CHIWAMBO AUSI R, TEKU UNIVERSITY, 2012

Tuesday, May 8, 2012

IS IT UN PERFORM ITS WORK EFFECTIVELY?

Nashangaa maamuzi ya UN kwa kutoichukulia SYRIA maamuzi yaliyo na tija.leo nazungmzia sala la UN (united Nation) juu ya mzozo wa Syria. ukweli ni kwamba hii UN inaonekana kama kivuli yaani ipo tu kwenye karatasi. hali ya Syria leo hii ni mbaya na yule Rais Asadi anaendeleza kali ya kusema hawezi kukaa meza moja na magaidi katika nchi yake (chanzo cha habari ni DW swahili saa 12.00, DW news).

wale ni waasi na nchi za magharibi wanawaona kama hawana makosa. hivi katika nchi zao ikitokea kuna makundi ya wapinzani yanayolenga kuleta mabadiliko kama yale ya waasi kule Syria na Libya watawaunga mkono au watawamaliza kwa kufagia virungu? UN ipo ipo tu. leo mamia ya watu wanauawa lakini hiki chombo kinaamini wale waangalizi watafanya kazi ipasavyo. huu ni uhuni wa hali ya juu.

kwanini mtu asizuiwe kufanya mauaji. kule Libya walikwenda haraka na majeshi ya yao ya NATO yakiongozwa na Mfaransa chini ya Rais aliyeshindwa uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya jumapili. kumbe ikiwa huku kwetu wanamvamia na majeshi yale yale ya majuu lakini ikitokea wale rafiki zao waarabu kama Syria wanawachekea. jamani nashangaa tunatoka wapi tunaelekea wapi na mwisho wake nini.

DW na VOA inatangaza kuwa wat wale inaonyesha ni vita ya wenyewe kwa wenyewe. hivi ninyi UN mnafanya kazi gani hadi watu wanauana wenyewe kwa wenyewe. unasikitisha sana kuona chombo kama hiki kuwa na ndoto kuwa watafanikiwa mbinu yao kumbe ni kupoteza muda. kauli iliyonaswa leo hii na vyombo vya habari mbalimbali inaonyesha hali inaelekea kuwa mbaya na Rais ataki kabisa kukaa meza moja na waasi.

chombo hiki kwa waafrica walio wengi pamoja na mimi naona kimeshindwa kazi maana huwezi kuwaacha wat wauane. kuna tofauti gani kati ya yale yaliyotokea Libya na Syria? hata ile mahakama yao naona pia ni kwa ajili yet sisi waafrica. wazungu kule ze hegggggggggggggggggggggggg no. wanakaa kimya. heb nirudi ndani ya mada husika iliyopo mezani kwa sasa. hivi zile goals zake zipo kwenye karatasi tu? naomba majibu wadau wenzangu. maana sielewi tunakwenda wapi? tunatoka wapi na hiki chombo maarufu.

sijamaliza lakini naishia hapo kwa kuwa wengi wamezngmza lakini mimi naona haya niliyozungumza yanatosha kwa leo. www.mwanaharakati.com

Saturday, April 7, 2012

MAENEO YA KANDA YA ZIWA. UNAWEZA KUSEMA UWANJA WA NDEGE, LAKINI SI UWANJA WA NDEGE BALI NI HALI YA UJANGWA
MAENEO YA NZEGA VIJIJINI.

NINI HATIMA YA BONGO MOVIES?

Npigo kubwa sana kwa industries ya muziki Tanzania baada ya kuondokewa na msanii maarufu Tanzania pamoja na Afica kwa ujumla. nini hatima ya industrial hiyo kwa sasa? je mikoba atalisi nani? hivi kweli kuna mtu aliyejitoa mhanga kama hayati kanumba?
mungu ndiye ajuaye. je tumkabidhi Rai-Vicent Kigosi au tumkabidhi JB. Muziki wa tanzania kwa sasa umekuja na sura mpya. hadi watoto walimpenda na aliwashirikisha katika movies zake. ukikumbuka ile filam ya The Big Dad, na Uncle JJ. mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. ameeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

ARUSHA NA TANZANIA YA LEO NA KESHO

Pigo Chadema

Thursday, 05 April 2012 10:56

http://www.mwananchi.co.tz/images/stories/lema-godbless-top.jpgLEMA AVULIWA UBUNGE ARUSHA MJINI, JAJI AMZUIA KUGOMBEA MIAKA MITANO, VILIO MAHAKAMANI
Waandishi Wetu, Arusha
MAKAHAMA Kuu Kanda ya Arusha,  imetengua matokeo ya ubunge yaliyompa ushindi mgombea wa Chadema, Godbless Lema baada ya kuridhika kuwa alitumia lugha ya kashfa na udhalilishaji dhidi ya aliyekuwa mpinzani wake katika uchaguzi huo wa mwaka 2010, Dk Batilda Burian.

Lema ni mbunge wa nne nchini kuvuliwa ubunge na mahakama katika kipindi cha miaka 16 iliyopita kutokana na kasoro zilizojitokeza katika mchakato wa uchaguzi.

Akisoma hukumu yake jana iliyochukua zaidi ya saa nzima, Jaji Gabriel
Rwakibarila alimtia hatiani Lema kwa makosa mawili kati ya manne
aliyokuwa akikabiliwa nayo, huku akitupa mawili kwa kukosa ushahidi.

Ndani ya ukumbi wa mahakama uliojaa wanachama, wafuasi na wapenzi wa Chadema, Jaji Rwakibarila alimvua ubunge Lema baada ya kuridhika na ushahidi kuwa alitumia maneno ya kashfa na ubaguzi wa jinsia dhidi ya aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk Batilda Burian.

Jaji Rwakibarila katika hukumu yake hiyo, pia alimwamuru Lema kulipa gharama za kesi hiyo na kwamba ana haki ya kukata rufaa ikiwa hajaridhika na hukumu hiyo.

Uamuzi wa Jaji huyo ni kama umetia doa shamrashamra za Chadema ambazo zilikuwa zikiendelea baada ya chama hicho kushinda kiti cha ubunge katika uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki, kupitia kwa mgombea wake, Joshua Nassari.

Makosa ya Lema
Lema alitiwa hatiani kwa kudaiwa kusema kuwa Dk Burian hakustahili kuchaguliwa kuwa mbunge kwa sababu mila na desturi za makabila ya Waarusha (Wamaasai na Wachaga), mwanamke hawezi kuongoza wazee.

Sababu ya pili aliyotumia Jaji kutengua ubunge wa Lema kutoa maneno ya kashfa dhidi ya Dk Burian kuwa ni mwanamke asiye mwaminifu, aliyezaa nje ya ndoa na alikuwa na mimba nyingine na bwana huyo aliyezaa naye ambaye siyo mumewe.

Jaji Rwakibarila alitupilia mbali madai mawili ya kutumia lugha na maneno yenye mwelekeo wa ubaguzi wa kidini na ubaguzi wa makazi.

Kuhusu ubaguzi wa kidini alikataa madai ya walalamikaji Mussa Mkanga,
Agness Mollel na Happy Kivuyo kuwa kauli ya Lema kuwataka wapiga kura wa Arusha kujihadhari na wanaovaa vitambaa na hijabu wasije kujikuta wanachagua Al Qaida kuwa haihusiani na dini ya Kiislamu.

“Mwanamke kuvaa kitambaa kichwani haina uhusiano wowote na dini ya
Kiislam wala Al Qaida kwani ni dhahiri wanawake wengi ambao baadhi yao
siyo Waislam wanavaa vitambaa. Kwanza ni heshima kwa wanawake kuvaa vilemba hivyo madai haya nayatupilia mbali,” alisema Jaji Rwakibarila katika hukumu yake.

Kuhusu tofauti ya ukaazi kati ya Lema na Dk Burian aliyedaiwa kuolewa
na kuishi Zanzibar, Jaji huyo alisema hoja hiyo isingeharibu wala kwenda
kinyume na maadili ya kampeni kwani kisheria Mtanzania ana haki ya
kuishi upande wowote wa Jamhuri ya Muungano, yaani Bara na Visiwani.

Katika shauri hilo namba 13/2010, wadai waliowakilishwa mahakamani na Mawakili Alute Mughwai na Modest Akida, waliomba mahakama kutengua matokeo yaliyompa ushindi Lema kwa madai kuwa alitumia lugha na kauli za matusi, kashfa na udhalilishaji dhidi ya Dk Burian wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita.

Jaji Rwakibarila alisema baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi 14 wa
upande wa wadai na wanne wa upande wa utetezi, aliridhika kuwa Lema alitamka maneno ya kibaguzi, kijinsia na kashfa dhidi ya Dk Burian katika mikutano yake minane ya kampeni kati ya mikutano zaidi ya 60 aliyofanya.

Kabla ya kuanza kusikilizwa mbele ya Jaji Rwakibarila, shauri hilo
lilikuwa mbele ya Jaji Aloyce Mujulizi aliyejitoa baada ya Lema kueleza kutokuwa na imani naye kutokana na wabunge wa Chadema kuwahi kuituhumu kampuni yake ya uwakili ya IMMA aliyokuwa akifanyia kazi
kabla ya kuteuliwa kuhusika na ufisadi wa akaunti ya EPA katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT)

Jaji Rwakibarila alianza kusikiliza shauri hilo mfululizo kuanzia mapema Februari kutokana na kutakiwa kulimazika kabla ya Mei 3, mwaka huu kutokana na mahitaji ya kisheria inayoelekeza kesi za uchaguzi zisikilizwe na kuamuliwa ndani ya mwaka mmoja tangu kufunguliwa.

Licha ya kuibuka washindi kwa uamuzi wa Jaji jana, wadai katika shauri
hilo pamoja na mawakili wao walionekana kupigwa bumbuwazi mahakamani bila kuamini kilichotokea hadi watu walipoanza kuondoka baada ya Jaji kutoka ndipo waliposimama na kuanza kukumbatiana na kupongezana.

Baada ya mwaka mmoja kukamilika Novemba, mwaka jana, Msajili wa Mahakama Kuu, Herbert George aliandika barua kwa Waziri mwenye dhamana ya sheria ambaye aliongeza kipindi cha ziada cha miezi sita
kinachomalizika Mei 3, mwaka huu.

Mkanganyiko kwenye hukumu

Jaji Rwakibarila kwa upande mwingine anadaiwa kujichanganya katika vifungu vya sheria alivyotumia katika uamuzi wake.

Akitoa uamuzi wake jana, Jaji huyo alisema Lema alithibitika kutenda kosa la kutumia maneno yasiyostahili kwenye kampeni zake za Uchaguzi Mkuu mwaka 2010.

Kwa kauli ya kisheria, Jaji alisema Lema anatiwa hatiani kwa kosa la
‘Illegal Campaign’ kwa kutoa kauli za kumbagua kijinsia Dk Burian
akitumia tofauti yao ya kimaumbile ya yeye kuwa mwanamme na mwenzake mwanamke aliposema mila na desturi za Waarusha na Wachaga haziruhusu mwanamke kuongoza wanaume.

Alisema hata kauli ya Lema kuwa Dk Burian siyo mwanamke mwaminifu
aliyezaa nje na kupata mimba nje ya ndoa ilikuwa ya kashfa dhidi ya
mgombea huyo wa CCM na kutafsiri kosa hilo kama ‘Illegal Campaign’
aliyosema inatosha kutengua matokeo ya uchaguzi.

Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi, makosa yote mawili yanaangukia
kwenye kifungu cha 108, kifungu kidogo cha pili aya ‘A’ ambayo
humruhusu aliyevuliwa ubunge kugombea kwenye uchaguzi mdogo
utakaoitishwa.

Lakini katika majumuisho ya hukumu yake, Jaji Rwakibarila alitumia
kifungu cha 114 cha sheria ya uchaguzi inayozungumzia “Illegal
Practice” ambayo yanaangukia kwenye makosa yanayohusiana na vitendo vya rushwa kwa wapiga kura, watendaji wa Serikali na watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Wakili wa Lema, Method Kimomogoro  alithibitisha utata huo na kusema atafuatilia kujua iwapo Jaji Rwakibarila alijichanga katika kutaja vifungu hivyo vyenye maana na adhabu tofauti kisheria.

“Anayehukumiwa kwa makosa yanayoangukia kwenye kifungu cha 108 (II) (A) kama ilivyotokea kwa mteja wangu (Lema) anaruhusiwa kugombea kwenye uchaguzi, lakini kwa mshangao wakati akihitimisha hukumu yake jaji alitaja kifungu cha 114 ambacho ni kinyume na makosa aliyokutwa nayo Lema,” alidai Wakili Kimomogoro.

Bila kutaka kuingia kwa undani katika suala hilo hadi atakapopata
nakala ya hukumu hiyo, Kimomogoro alidai hadi jana jioni alikuwa
hajapata maelekezo yoyote kutoka kwa mteja wake kuhusu hatua za
kuchukua dhidi ya uamuzi huo.

Kimomogoro alieleza kuwa iwapo hukumu hiyoitaachwa kubakia kwenye kifungu hicho cha 114 ina maana mteja wake Lema hataruhusiwa kugombea ubunge kwa kipindi kisichopungua miaka mitano, jambo ambalo siyo haki kwa sababu hakushtakiwa wala kukutwa na hatia ya kujihusisha na rushwa wakati wa kampeni.

Kwa upande wake, wakili wa wadai Alute Mughwai aliyekuwa akisaidianana Modest Akida alieleza kuridhishwa na uamuzi huo ingawa aliahidi kuwasiliana na wateja wake kuangalia uwezekano wa kukatia rufaa hoja mbili za ubaguzi kimakaazi na kidini zilizotupwa na mahakama.

Happy Kivuyo aliyekuwa mdai wa tatu katika shauri hilo nambo 13/2010
alieleza kufurahishwa na hukumu hiyo aliyodai imewatendea haki wote
waliochukizwa na matusi, kashfa na udhalilishaji uliofanywa na Lema
dhidi ya Dk Burian.

Kauli ya Mbowe
Mwenyekiti wa  Chadema, Freeman Mbowe, amevitaka vyombo vyenye Mamlaka ya Maamuzi nchini, ikiwepo Mahakama kusoma alama za nyakati kabla ya kutoa uamuzi ambao unaweza kusababisha nchi kuingia katika machafuko.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi za Chadema Mkoa wa Arusha, eneo la Ngarenaro, kuhusu hukumu ya Jaji Rwakibarila, Mbowe alisema ni hatari pale watu wanapoanza kutilia shaka vyombo vya uamuzi kama Mahakama Kuu.

“Sitaki kuingilia uamuzi ya mahakama, lakini ni kweli kuwa uamuzi wa hukumu hii ulivuja hata kabla ya kusomwa, tulipewa taarifa za ubunge wa Lema kutenguliwa, sasa hili ni jambo la hatari kama tutaendelea kuvujisha uamuzi wa kisheria, nchi inaweza kuingia kwenye machafuko pale watawala wanapoingilia vyombo vya kisheria,”alisema Mbowe.

Alisema Serikali na vyombo vingine vyenye Mamlaka, ni lazima wajue kuwa, enzi za kuwaburuza watu zimepitwa na wakati.

“Mahakama zisifikiri zinaweza kufanya kila ambacho zinataka bila kuzingatia, sheria, taratibu na matakwa ya  umma, mimi sitaki tukife huko,”alisema Mbowe.

Alisema katika kesi hiyo ya Lema, wanaamini uamuzi ya mahakama umeingiliwa na chombo kingine jambo ambalo ni hatari katika utawala wa Sheria.

Kukata rufani
Kuhusu Chadema kuukatia rufaa uamuzi wa Lema kuvuliwa ubunge, Mbowe alisema bado wanasubiri nakala ya hukumu ya kesi hiyo na wanafanya majadiliano kupitia mawakili wa chama hicho na viongozi wengine na kisha watatoa uamuzi ambao utatangazwa kesho Jumamosi kwenye mkutano wa hadhara.

Mbowe alisema, ingawa wananchi wengi wa Arusha wanataka kurejewa haraka kwa uchaguzi, lakini, hawafahamu kama Mbunge wao Lema, kulingana na hukumu hiyo ataruhusiwi kugombea tena.

“Kabla ya kufikia uamuzi wowote  tumeona ni busara kwanza, tukae kwani Lema ambaye wanamtaka kwa hukumu hii ni lazima tukate rufani,”alisema Mbowe.

Hata hivyo, aliwaomba wananchi wa Arusha, kutulia kwa sasa na kutofanya vurugu zozote ili kuthibitisha Chadema sio chama cha vurugu na ni chama cha wanademokrasia wa kweli.

Alisema katika mkutano wa Jumamosi, watatoa tamko la pamoja kama watakata rufani au watatoa nafasi kwa wanachama wengine wa Chadema kujitokeza kumrithi Lema.

Kabla ya kukutana na waandishi wa habari, Mbowe alizungumza na mamia ya wakazi wa Jiji la Arusha nje ya Uwanja wa ofisi za Chadema, ambao pia aliwataka kutulia wakati chama hicho kinatafakari uamuzi wa kuchukua.

Chaguzi zilizowahi kutenguliwa
Mwaka 1996 aliyekuwa mbunge wa Temeke, Ramadhani Ali Kihiyo alivuliwa ubunge baada ya Mahakama kumtia hatiani kwa kosa la kughushi cheti na nafasi yake ilichukuliwa na Augustine Mrema, wakati huo akiwa Mwenyekiti wa Chama cha NCCR- Mageuzi.

Vivyo hivyo Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba ilitengua ubunge wa aliyekuwa mbunge wa Biharamulo Magharibi kwa tiketi ya Chama Cha Tanzania Labour (TLP), Phares Kabuye.

Kabuye aliyefariki dunia kwa ajali ya gari akiwa njiani kuelekea jijini Dar es Salaam, alivuliwa ubunge baada ya mahakama kuthibitisha kuwa katika mchakato wa uchaguzi mwaka 2005, alimdhalilisha mgombea mwenzake, Anatoly Choya.

Desemba 28, 2007 Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, kupitia kwa Jaji Josephat Mchome ilitengua matokeo ya aliyekuwa mbunge wa Mwibara Charles Kajege kutokana na kutiwa hatia kwa rushwa.

Kesi ya kupinga matokeo ya hayo ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea wa jimbo hilo kupitia TLP, Mtamwega Mgaywa, (TLP) aliyeshindwa katika Uchaguzi Mkuu wa 2005.

Hata hivyo, Septemba 25, 2009, Mahakama ya Rufaa chini ya majaji watatu, wakiongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania wakati huo, Agustino Ramadhani, January Msofe na Jaji Mbaruku, walimrejeshea Kajege ubunge kutokana na rufaa aliyokata dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu.

Habari hii imeandaliwa na Mussa Juma, Arusha, Peter Saramba, Moses Mashalla
CHANZO CHA HABARI NI GAZETI LA MWANANCHI
NA CHIWAMBO AUSI R.
Karbu siku mzima Arusha na Tanzania kwa ujumla siku tatu zilizopita vichwa vya watu viligonga mwamba kuhusiana na kitendo cha mahakama kubatilisha ubunge wa Mh. Godbless Lema. Tukumbuke kwamba katika nchi yetu ni ya demokrasia. Na ikumbukwe kuwa katika nchi ya Tanzania kuna mihimili mikuu mitatu ambayo ni Serikali, mahakama na bunge. Hivyo basi hukumu ya mahakama haiwezi kuingiliwa na muhimili mungine. Hivyo ule usema wa lema kuwa zilikuwa ni njama za serikali ikuru ya Tanzania ilikanusha maneno yake kama inavyoonekana hapa chini katika barua iliyoandaliwa na ikuru;

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katika mahojiano yake leo, Alhamisi, Aprili 5, 2012, na Redio One, ikiwa ni kauli yake ya kwanza baada ya Mahakama Kuu ya Arusha kutangaza kumvua ubunge, aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Bwana Godbless Lema, amedai kwa jazba sana kuwa hukumu ya Mheshimiwa Jaji Gabriel Rwakibalira imetokana na maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Ikulu.
Kauli hii ya Bwana Lema ni upuuzi. Siyo Mheshimiwa Rais Kikwete wala Ikulu imeingilia kati kesi yake kwa namna yoyote ile, iwe ni kwa kupiga simu ama kuzungumza na Mheshimiwa Jaji Rwakibalira.
Kwa hakika, haijapata kutokea Mheshimiwa Kikwete, tokea alipoingia madarakani, Desemba 21, 2005, akaingilia, kwa namna yoyote ile, mwenendo wa kesi yoyote ile katika Mahakama yoyote na ya ngazi yoyote katika Tanzania. Na wala hakusudii kufanya hivyo wakati wote wa muda wake uliobakia wa uongozi. Siyo kazi ya Rais kutoa hukumu ama kuelekeza namna ya kutoa hukumu katika kesi zilizoko Mahakamani. Rais hana madaraka wala mamlaka hayo.
Aidha, kauli ya Bwana Lema ni ukosefu mkubwa wa adabu na heshima kwa Mahakama ambao ni Muhimili Huru usioingiliwa na Serikali ama na Muhimili mwingine katika maamuzi yake. Bwana Lema amekuwa kiongozi kwa muda sasa, hivyo ni lazima atambue jambo hili kubwa na muhimu katika mfumo mzima wa utawala wa nchi yetu.
Ni jambo lisilokuwa na mshiko wala tija, na kwa kweli ni bahati mbaya, kwamba Bwana Lema anajaribu kuingiza mambo yasiyohusika katika jambo la dhahiri kabisa kuwa ni la kisheria ambalo msingi ni hoja na maelezo mahakamani.
Bwana Lema asitafute visingizio kwa yaliyomfika kwa sababu hakuna mtu mwingine wa kumbebea msalaba huu.  Badala ya kutafuta mchawi asiyekuwepo, ni vyema Bwana Lema angekaa chini na kuangalia ni sababu zipi za kisheria zilizomfanya ashindwe na kama ameridhika kuwa hakutendewa haki akate rufani kwa mujibu wa sheria na taratibu. Tunaomba wananchi wampuuze.  Ameshindwa kesi kwa makosa yake aliyofanya hana mtu wa kumlaumu bali ajilaumu mwenyewe.

Mwisho.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
05 Aprili, 2012