Wachezaji wa Spurs, Sandro (kushoto)
na Christian Eriksen wakiwa wanyonge baada ya kutolewa katika Europa League
jana na Benfica
Na BIN ZUBEIRY
ENGLAND haitakuwa na timu katika Robo
Fainali ya Europa League kufuatia Tottenham Hotspur jana kutolewa na Benfica ya
Ureno kwa jumla ya mabao 5-3, baada ya usiku wa jana kulazimishwa sare ya
kufungana mabao 2-2 Uwanja wa Luz.
Spurs ilifungwa 3-1 nyumbani katika
mchezo wa kwanza na sasa inaungana na Swansea kuipa mkono wa kwaheri michuano
hiyo.
Katika mechi nyingine za Hatua ya 16
Bora ya michuano hiyo, Valencia imesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-0
dhidi ya Ludogorets baada ya jana kushinda 1-0 nyumbani, ikianza kushinda 3-0
ugenini, wakati Napoli imeaga kwa kipigo cha jumla cha 3-2 kufuatia jana
kufungwa 1-0 na Porto ikitoka kulazimishwa sare ya 2-2 nyumbani katika mchezo
wa kwanza.
FC Basel imesonga mbele kwa ushindi
wa jumla wa 2-1 dhidi ya Salzburg baada ya sare ya 0-0 jana nyumbani, ikitoka
kushinda 2-1 katika mchezo wa kwanza ugenini, wakati Anzhi nayo imeaga kwa
kipigo cha jumla cha 1-0 walichokipata katika mchezo wa kwanza ugenini na jana
kutoa sare ya bila kufungana.
Viktoria Plzen imeaga kwa jumla ya
mabao 5-3 dhidi ya Olympique Lyon baada ya jana kushinda 2-1, wakati mchezo wa
kwanza ilifungwa 4-1, Fiorentina imetolewa kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya jana
kufungwa 1-0 na Juventus nyumbani, ikitoka kulazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na
Sevilla imefuzu kwa penalti baada ya sare ya jumla ya 2-2 na Real Betis, kila
timu ikishinda 2-0 nyumbani kwake
Chanzo: Mjengwa

No comments:
Post a Comment