Sunday, March 30, 2014

SAFARI YANGU YA MATESO TUNDURU-SONGEA NA Chiwambo's Blog


Hii Ndio Barabara ya Mtwara Korido maarufu kwa jina la Tunduru-Songea
MAOMBI YA WANATUNDURU NI KUONDOKANA NA HII KERO
                          Miongoni mwa hao ni Mwenyekiti wa Chiwambo's Blog Ndugu Ausi Chiwambo.
 Picha Hii ni Barabara ya Tunduru Songea Mbele ya kijiji cha Namwinyu huko Wilayani Tunduru.
               Safari Wakati wa mvua zinakuwa hivi kama muonavyo kwenye hiyo TDI Defenda. Hapa ilikuwa baada ya kuharibikiwa na gari.
 Picha juu ni Stendi ya Namtumbo tayari kwa kuanza safari ya Tunduru
Baada ya Kuharibikiwa na Gari. Ausi Chiwambo ni Mwenye Shati jeupe na kachuchumaa chini kuonyesha hali imekuwa Mbaya


Ndivyo ilivyo barabara ya Tunduru-Songea, Kodi za wananchi zna kwenda wapi, makaa ya mawe Mbinga, uranium Namtumbo, madini aina nyingi 2nduru, gesi Mtwara, mazao ya chakula na biashara asilimia kubwa huzalishwa kusini, Nini hatima ya Mtwara coridal? Tunduru,Masasi na Mbambabay wataijua lami lini? 

Serikali inamtazamo gani kutanua majiji sehemu nyingine? Kwanini kung'ang'ania kuhamishia malighafi Dar badala ya kujenga viwanda pale malighali yalipo? Serikali isaidie watu kupata ajira kutokana na malighafi zilizo kwenye mazingira yao na co kuhamisha, wananchi hunyanyasika kwa maamuzi yasiyo ya ridhaa yao.

UKWELI BARABARA YA TUNDURU-SONGEA NI HATARI KWA USALAMA WA ABIRIA.  KULALA NJIANI NI JAMBO LA KAWAIDA NYAKATI ZA MVUA KALI. Picha na Ausi Chiwambo-Tunduru

1 comment:

PHILIPO DE SPEAR said...

unaongelea serikali ipi hyo mkuu ? Hakuna serikali BONGO , serikali iliyopo haina watu wenye kujua vipaumbele mzee , hyo coridor nimeanz kuisikia tangu enzi za DK MTAZAMA GAMA
mpaka leo hakuna jipya