Tuesday, March 25, 2014

Wahitimu wa elimu juu hawana uelewa na ufahamu wa kutosha wa kile walichokisomea

BAADHI ya wahitimu wa elimu juu hawana uelewa na ufahamu wa kutosha wa kile walichokisomea na mambo yanayoendelea kwenye mazingira husika.

Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Riziki Abrahamu, alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.

“Ubora wa wahitimu wanaomba kazi kupitia chombo hiki wamekuwa hawana uwezo wa kitaalamu, ufahamu, kutotilia maanani vigezo na masharti ya tangazo, kutojiamini, uwezo mdogo wa mawasiliano ikiwemo matumizi ya lugha sahihi na kuamini kuwa vyeti vinaweza kuwasaidia kupata kazi kwa urahisi,” alisema.

Alisema wahitimu wengi kutokuwa na maandalizi sahihi na kukosa sifa halali za kitaaluma huchangia kughushi baadhi ya sifa kwa lengo la kujipatia ajira.

“Hali hii inatisha na inatudhirihishia kwamba wahitimu wetu wanasoma kwa kufuata mkumbo, lakini si kuelewa kile wanachosomea,” alisema.

Chanzo: Tanzania Daima

No comments: