Benki ya dunia imeidhinisha msaada wa
kitita cha dola milioni sabini na saba kuisaidia Jamuhuri ya kidemokrasi ya
Kongo kuendeleaza mradi wa bwawa la umeme.
Benki ya dunia imesema pesa hizo ,
pamoja na dola milioni thelathini na tatu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika
zitadhamini uchunguzi wa kina wa athari za kimazingira katika bwawa umeme la
Inga na kuhakikisha mradi huo unaimarika .
Makampuni matatu ya kimataifa
yamepata kandarasi ya kujenga mabwawa mengine kutoka kwa bwawa hilo
yajulikanayo kama Inga Three.
Waziri mkuu wa Kongo Augustin Matata
Ponyo amesema mradi huo ni wa mafanikio makubwa kwa Afrika katika karne ya 21 .
Waandishi wa habari wanasema mabwawa
mawili yaliyopo kwa sasa yalijengwa miongo kadhaa na yameharibika baada ya
kutelekezwa na ukosefu wa uwekezaji katika miundo mbinu hiyo muhimu.
Chanzo: BBC Swahili

No comments:
Post a Comment