Tuesday, March 25, 2014

VITA YA VYOMBO VYA HABARI TANZANIA ITATUFIKISHA KUBAYA


 Jaji Joseph Warioba                                                                                      Rais Jakaya M. Kikwete


NA Ausi Chiwambo
Kwa Ufupi
Hotuba ya Rais Kikwete iliyotolewa siku chache zilizopita imeleta mvutano miongoni mwa watanzania huku vyombo vya habari navyo vikiwa vimegawanyika katika pande mbili yaani vinavyounga serikali mbili na vile vinavyounga serikali tatu.

HABARI KAMILI
Nchi ya Tanzania inapita kipindi kigumu sana hasa wakati huu Bungemaalumu  la katiba likiendelea na kazi zake huku kukiwa na mvutano wa wazi kati ya wanaopina serikali mbili na wanaopenda serikali tatu. Mvutano huu umeanza kuwa mkubwa hasa baada ya Rais Wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya M. Kikwete kutoa hotuba yake iliyolenga haja ya kuwa na serikali tatu.

Mara baada ya kutolewa kwa hotuba hiyo Watanzania wamegawanywa katika makundi mawili yaani wale wanao unga serikali mbili na wale wanaopendekeza serikali tatu. Vita hivyo vimeendelea kusikika si tu katika ndani ya Bunge Maalumu la Katiba bali hata vyombo vya habari vimeingia katika mvutano mkali huku baadhi ya vyombo vya habari vikirusha kwa mtanzamo wa serikali mbili na vingine serikali mbili.

Ikumbukwe kwamba sisi sote ni Watanzania na lengo letu ni kupata katiba mpya,hivyo vyombo vya habari kwa tafsiri ya neon la kiingereza  “The voice of the voiceless”  nikimaanisha Kipaza sauti kwa wale wasiojiweza hasa wananchi havina budi kujenga maslahi ya Watanzania kwanza na si kuingia katika vita baina ya vyombo hivyo vya habari kama vile Magazeti, Radio, pamoja na Televisheni.

Kutokana na kinachoendelea inaonyesha wazi kuwa hata taaluma yetu ya uandishi wa habari ni ya Kikanyanja maana tupo tayari kuingia mikononi mwa wanasiasa na sio kuangalia maslahi ya Watanzania. Waandishi tujiulize swali moja kuwa hivi taaluma yetu ni kwa ajili ya maslahi ya Watanzania au kwa maslaya ya wanasiasa na wamiliki wa vyombo vya habari?

TUME YA KUKUSANYA MAONI YA WATANZANIA
Hoja ya kuwepo kwa katiba mpya kwa mara ya kwanza ilisikika kutoka kwa Rais Kikwete kuwa kuna haja ya Watanzania ijapokuwa haikuwepo katika Ilani ya Uchaguzi wa CCM (Chama Cha Mapinduzi) bali ilikuwa kwa busara za Rais peke yake. Hii yote ilitokana na msukumo mzito kutoka vyama pinzani vikiwemo Chama cha CUF, NCCR Mageuzi, na Chadema.

Baada ya hoja hizo Rais Kikwete aliamua kutoa hoja ya kuwa na mchakato wa katiba mpya. Tume ya kukusanya maoni ya Wananchi iliundwa ikiwa na lengo la kupata maoni ya Watanzania ili kupata katiba ya Watanzania na si kama katiba ya mwaka 1977 iliyotungwa na jopo la watu 20. Hivyo kwa busara za Rais aliona kuna umuhimu wa kupata maoni ya Watanzania ili waseme aina ya katiba wanayoipenda.

Tume ilianza kazi zake na kuweza kuzunguka nchi nzima na kupata rasimu ya kwanza nay a pili ikiwa na maoni ya Watanzania wa kila hali. Tume imamaliza kazi yake na kazi iliyopo ni ya Wabunge kati ya kusaliti maoni ya Watanzania na kuingiza yao au kuyafanyia kazi maoni ya watanzania. Picha na kitendawili kilianza kuonekana wiki moja iliyopita mara baada ya Jaji Joseph Warioba kutoa hotuba yake ndani ya Bunge la Katiba na kueleza Watanzania Wamependekeza nini huku msimamo wao ni serikali Tatu.

Na ikumbukwe kwamba Tume mbalimbali zilizoundwa hapo nyuma  ikiwemo ya Jaji Nyarali zilipendekeza kuwa Watanzania wanahitaji serikali tatau yaani ya Tanganyika, Zanzibar, pamoja nay a Muungano. Siku ya  ijumaa ya wiki iliyopita Rais Kikwete naye alitoa hotuba yake ili kufungua bunge. Hotuba ya Rais ilipendekeza umuhimu wa kuwa na serikali mbili ile hali tume ilipendekeza serikali tatu.

Hapo ndipo  Watanzania wanaposhuhudia mvutano wa Wabunge ndani ya Bunge la Katiba, Wanaharakati na Wasomi mbalimbali huku hata vyombo vya habari navyo vikiwa vimegawanyika mapande mapande hasa baada ya hotuba ya Rais kutolewa.

Ni maoni yangu kwamba Watanzania wa leo wanatambua kila kitu kinachoendelea. Na kuja na katiba mbaya ni mwanzo wa kuanza mchakato wa katiba mpya nyingine itayokuwa ya wananchi na sio ya chama Fulani.

Imeandikwa na
Ausi Chiwambo

No comments: